Viongozi wa Serikali na Chama Tawala CCM wamefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma
Lengo la Ziara hii ni kuona namna miradi ya maendeleo inavyotekelezwa na kutatua Kero mbalimbali za Wananchi .
Akizungumza mara baada ya kutembelea miradi hiyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyasa Komred Abel Komba ameridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Zahanati ya Nkaya, madarasa ya Shule ya msingi Ndumbi, Barabara ya Liweta hadi Mpopoma na Mradi wa Maji wa Ngumbo unaokwenda kutatua Kero ya Wananchi wa vijiji sita vilivyopo katika kata za Ngumbo na Liwundi.
Akizungumza katika Mradi wa shule ya Sekondari Mkali,Komba amewataka Wananchi na viongozi kuhakikisha wanaongeza Kasi ya utekelezaji wa Mradi huo ili uanze kuwahudumia wananchi.
Amemshukuru na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kupeleka fedha nyingi zinazotekeleza Miradi mbalimbali katika wilaya ya Nyasa.
Amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Peres Magiri na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Khalid Khalif kwa kusimamia vema utekelezaji wa miradi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.