• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

VITUO 43 vya tohara Ruvuma kupewa vikwambi

Imewekwa kuanzia tarehe: August 2nd, 2024

Na Gustaph Swai-RS Ruvuma

Vituo 43 vinavyotoa huduma za tohara katika Mkoa wa Ruvuma vitakabidhiwa vishikwambi 84 vyenye thamani ya shilingi milioni 39 vilivyotolewa na Taasisi ya HJF Medical Research International.

Vishikwambi hivyo vimekabidhiwa na Mwakilishi wa Taasisi hiyo, Dr. Joshua Mwakanyamale, kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Dr. Louis Chomboko, katika hafla iliyofanyika  kwenye ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa mjini Songea.

Akizungumza kabla ya kukabidhiwa vishikwambi hiyo,Dr.Chombo amesema vishikwambi hivyo vimetolewa kwa ajili ya kusaidia kutekeleza afua ya toharakinga kwa wanaume ambayo inasaidia kuzuia maambukizi ya VVU kwa asilimia 60.

 "Vishikwambi hivi vimekuja wakati muafaka na sasa vitaenda kugawiwa kwa vituo 43 kwa watoa huduma na waelimishaji rika ili kuweza kukusanya takwimu ya wale wote ambao tutakuwa tunawafikia kwa huduma ya tohara," amesema Dr. Chomboko.

Amebainisha kuwa Mkoa wa Ruvuma unashirikiana na Shirika la HJF -Medical Research International kwa ajili ya utekelezaji wa afua hiyo ili kuwezesha ufuatiliaji  na kufikia wateja Zaidi ya 35,000 katika Mkoa ambapo hadi sasa wateja Zaidi ya asilimia 70 wamefikiwa.

Naye Mwakilishi wa Shirika hilo ambaye pia ni Msimamizi wa Tohara katika Mkoa wa Ruvuma Dr.Joshua Mwakanyamale amesema Shirika hilo linafanya kazi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Mbeya,Rukwa,Songwe,Ruvuma na Katavi.

Dr.Mwakanyamale amesema vishikwambi hivyo vitarahisisha utunzaji wa taarifa kwani vinatumia mfumo na teknolojia ya kisasa wa kutunza kumbukumbu ambao ni rahisi zaidi tofauti na ule wa karatasi.

Amesisitiza kuwa vishikwambi hivyo vitawawezesha watoa huduma kuhifadhi taarifa kwa usalama zaidi na kuwezesha taarifa hizo kupatikana kwa urahisi zaidi pale zinapohitajika.
Ugawaji wa vishikwambi kwa watumishi wa umma  katika Mkoa wa Ruvuma umekuwa endelevu ambapo serikali imeshatoa vifaa hivyo kwa Walimu wote wa Mkoa wa Ruvuma.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.