• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

VIVUTIO vya Utalii Kusini vitangazwe kwa nguvu zote

Imewekwa kuanzia tarehe: July 31st, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa rai kwa wadau wa watalii kuvitangaza vivutio vilivyopo ukanda wa kusini ili kufungua milango ya uwekezaji.

Ametoa rai hiyo wakati anafunga tamasha la  Majimaji Selebuka ambalo limefanyika kwa siku nane kwenye uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea.

“Tumezoea sana kutangaza vivutio kutoka kaskazini na  fukwe zilizopo Mashariki mwa nchi yetu, uwekezaji kusini unahitaji juhudi za pamoja wadau na wananchi wa Kusini ili  Southern Circuit yaanik Mzunguko wa Kusini kwa hakika utangazwe vema’’,alisisitiza  RC Ibuge.

Amesema kinachotafutwa hivi sasa ni kuongeza mapato kupitia sekta ya utalii na kuhakikisha kuna uendelevu wa kutambulisha vivutio vya kusini Duniani.

Brigedia Jenerali Ibuge amesema kuna soko kubwa la sekta ya utalii hivyo  juhudi kubwa katika kutangaza vivutio vya utalii zinaweza kuongeza uthaminishaji wa maliasili zilizopo na kuongeza kipato kwa wabunifu na wananchi.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kulitendea haki tamasha la Majimaji Selebuka mwaka huu ambapo ameagiza kuongeza juhudi zaidi katika kuhakikisha matamasha yajayo  yanakuwa na ushiriki mkubwa na kuongeza vikundi vya ushiriki kutoka mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara.

Katika Hatua nyingine RC Ibuge amewakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na UVIKO 19 kwa kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na wataalam wa afya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindii Mheshimiwa Zainabu Telaki akizungumza kwenye tamasha hilo  ametoa rai kwa wadau wa utalii kuhakikisha kuwa vivutio vyote vilivyopo kwenye mikoa mitatu ya kusini vinatangazwa kwenye luninga zote zilizopo nchini ili kufungua fursa za utalii kusini.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema akizungumza kwenye tamasha hilo amesisitiza vivutio adimu vya utalii vilivyopo kusini  ambavyo havipatikani sehemu nyingine duniani  vitangazwe kitaifa na kimataifa kuvutia wawekezaji.

Mgema ametoa rai kwa Bodi ya Utalii Tanzania kuhakikisha kuwa vivutio vya kusini vinakuwa sehemu ya vivutio vinavyotangazwa ili watalii wengi waweze kufika mikoa ya kusini kuangalia vivutio hivyo.

Amesema serikali tayari imeimarisha miumbombonu katika mikoa ya kusini hivyo watalii wanaweza kufika kusini kwa kutumia usafiri wa anga,barabara na majini.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa  wa Ruvuma

Julai 31,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.