Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amewasisitiza waandishi wa habari kuendelea kuyazingatia maadili ya uahandishi wa habari na kuwaelimisha wengine ambao wanakiuka maadili hayo.
Ameyasema hayo wakati akifungua Semina ya kijamii kuhusu kukuza uhuru wa kujieleza iliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa, Songea (HOMSO) mjini Songea, ambayo iliandaliwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Ruvuma (RPC).
"Wale ambao mnawaona wanaenda kinyume na sheria zenu msiwaone ni maadui, endeleeni kuwakumbusha, endeleeni kuwarudisha kwenye mstari ili muendelee kuijenga tasnia ya habari katika viwango vya juu vya thamani, wachache wasiwaharibie," alisema Kanali Ahmed.
Amewakumbusha waandishi wa habari kuendelea kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu ili kuwachagua viongozi ambao watashirikiana na Serikali kuleta maendeleo kwenye Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Kupitia Semina hiyo iliyowakutanisha wadau kutoka taasisi za kijamii, vyama vya siasa, viongozi kutoka Serikalini na dini pamoja na watu binafsi wenye ushawishi katika jamii, Kanali Ahmed amesema anawapongeza na anatambua kazi kubwa zinazofanywa na waandishi wa habari ya kuwahabarisha wananchi, hivyo ataendelea kushirikiana nao kuhakikisha kazi hiyo wanaifanya kwa mafanikio makubwa.
Uhuru wa kujieleza unapaswa kutumika kwa uwajibikaji, kuhakikisha maoni yanayotolewa hayavunji sheria wala kuumiza wengine, ni muhimu kuzingatia mipaka.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.