• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WACHIMBAJI madini wafurahishwa na elimu ya sensa

Imewekwa kuanzia tarehe: August 25th, 2022

WACHIMBAJI wadogo wa madini ya vito na dhahabu mkoani Ruvuma,wameiomba Serikali kupeleka elimu juu ya umuhimu wa sensa ya watu na makazi ili wachimbaji wote  washiriki zoezi hilo kwa  kutoa taarifa sahihi zitakazowezesha kufanikisha lengo la serikali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  wachimbaji hao walisema, kutokana na mazingira ya kazi zao ni vigumu kwa  baadhi ya wachimba kushiriki vyema kwa kuwa  bado hawajapa elimu  yoyote kuhusu kuwepo kwa sensa na umuhimu wake.

Makamu mwenyekiti wa  wachimbaji  madini mkoa wa Ruvuma(Ruvrema) Kassim Pazi alisema,baadhi ya wachimbaji wanaishi na kufanya kazi kwenye maeneo magumu yasiofikika kwa urahisi na wengine hawajafika kwenye vijiji au mjini kwa zaidi ya miaka mitano kwa hiyo itakuwa vigumu kuwapata.

Kwa mujibu wa Pazi ni kwamba,njia pekee itakayowezesha wachimbaji wengi kushiriki sensa ya mwaka 2022  ni viongozi wa serikali na watu waliopewa dhamana ya kuratibu  na kusimamia kazi hiyo, kwenda moja kwa moja katika maeneo ya machimbo ili  kutoa elimu kabla ya siku iliyopangwa kufanyika kwa zoezi hilo.

Pazi alisema katika maeneo hayo hakuna mawasiliano yoyote, kwa hiyo ni vigumu  baadhi yao kushiriki  kwa kuwa wako kwenye machimbo  kwa muda mrefu,hivyo sio rahisi kupata taarifa zozote na  hadi sasa hawaelewi faida ya zoezi hilo na umuhimu wake.

Pazi  ambaye  pia ni makamu mwenyekiti  wa kamati ya madini na viwanda nchini(Femata)alisema, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la  kupata idadi ya watu wote waliopo hapa nchini wakiwamo wachimbaji wa madini ili kupata taarifa muhimu zitakazowezesha kupanga mipango yake ya maendeleo.

Alisema, viongozi wa chama cha wachimbaji wilaya ya Tunduru na mkoa  wako tayari  kuisaidia serikali kufanikisha zoezi hilo, lakini hadi sasa serikali haijawashirikisha kama ilivyofanya kwa makundi mengine ya kijamii.Alisema,matarajio ya wachimbaji katika sensa ya mwaka huu serikali kupitia wizara ya madini itaweka dodoso litakalosaidia kukusanya taarifa za wachimbaji wa madini ili kuweza kujua mahitaji yao na kuwahimiza wachimbaji wote kutoa ushirikiano na  taarifa zao kwa usahihi.

Aidha,ameishukuru serikali kupitia wizara ya madini kwa uamuzi wa kujenga masoko ya madini mkoani Ruvuma ambayo yamewezesha wachimbaji wadogo hasa wa madini ya vito kupata sehemu ya uhakika na kuuza madini yao bila kudhurumiwa.

Mchimbaji wa madini kutoka wilaya ya Tunduru Ndwela Msuya,ameiomba serikali kuweka nguvu kubwa  maeneo ya machimbo ili siku ya sensa ikiwezekana wachimbaji  wakae sehemu moja  ili makarani  waweze kutekeleza majukumu yao na wachimbaji wapate nafasi ya kushiriki zoezi hilo muhimu kwa uchumi wa nchi yetu.

Msuya alisema,kama serikali haitajipanga vizuri  na kutoyashirikisha baadhi ya makundi  hasa yanayofanya shughuli zao kwenye maeneo magumu na yasio rasmi,kuna hatari ya kutowafikia watu wote siku ya sensa.

“naiomba serikali ituangalie sana sisi wachimbaji wadogo kwani tumesahaulika kwa muda mrefu sana, lazima  itambue kuwa Tunduru kuna wachimbaji wengi wa madini ambao wako tayari kuhesabiwa katika sensa mwaka 2022”alisema Msuya.

Msuya,ameipongeza serikali kujenga masoko  hayo ambayo yamesaidia sana wachimbaji wadogo kuuza madini yao kwa urahisi tofauti na siku za nyuma ambapo walilazimika kuuza kwa kutumia vipimi visivyo rasmi.

Alisema,kujengwa na kufunguliwa kwa masoko ya madini  wilayani Tunduru, kumewezesha kuongezeka kwa wanunuzi wengi kutoka ndani na nje ya nchi na kuwataka wachimbaji wadogo kutumia masoko hayo kuuza madini badala ya kutumia masoko ya mitaani.

Mchimbaji  Abdala Jumanne, amewaomba wachimbaji wenzake  kushiriki zoezi hilo kwani ni jambo muhimu ili serikali iweze kupata idadi sahihi ya watu wake  ili kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwamo makundi yenyemahitaji maalum kama vile watu wenye ulemavu,watoto,wanawake na vijana.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.