Wadau wa kilimo, wakulima, na wataalam wa upimaji wa udongo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) wamefanya kikao cha kujadili uzalishaji wa zao la soya na upimaji afya ya ndogo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Cottage Heritage mjini Songea.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Mary Makondo amefungua kikao hiko na kueleza namna serikali ilivyotoa kipaumbele katika sekta ya kilimo na jinsi ilivyojipanga kuongeza uzalishaji wa mazao na bidhaa za kilimo.
"Serikali imejipanga kuongeza uzalishaji, uchakataji na usafirishaji nje wa mazao ya kilimo na kugawa vitendea kazi kwa Maafisa ugani."alisema
Katibu Tawala huyo amewaagiza wakuu wa Idara kuendelea kusimamia zoezi la upimaji wa udongo na kuhakikisha maafisa ugani wanatekeleza malengo yaliyokusudiwa.
Naye Mtafiti wa Udongo kutoka TARI, Watson Matamwa, amesema hadi sasa afya ya udongo imepimwa Zaidi ya mikoa 15 na kwamba udongo wa Mkoa wa Ruvuma umepungua rutuba na eneo kubwa la kilimo lina udongo wenye asidi nyingi, hali ambayo inasababisha kupungua kwa uzalishaji wa mazao.
Matamwa ameitaja Halmashauri ya Madaba wilayani Songea kuwa ina udongo wenye asidi kwa kiasi kikubwa, hali inayosababisha kuongezeka kwa matumizi ya mbolea na kushindwa kufikia malengo ya uzalishaji yaliyowekwa na serikali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.