• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAFANYABIASHARA Ruvuma walivyodhamiria kushiriki maonesho ya bidhaa za viwanda Desemba 2020

Imewekwa kuanzia tarehe: October 18th, 2020


WAFANYABIASHARA wa Mkoa wa Ruvuma wamepitisha azimio la kushiriki kwa mara ya kwanza kwenye maonesho ya Tano ya bidhaa za viwanda vya Tanzania ambayo yanatarajia  kufanyika katika viwanja vya Mwl.J.K.Nyerere Dar es salaam kuanzia Desemba 3 hadi 9 mwaka huu.

Azimio  hilo limepitishwa katika kikao cha wafanyabiashara wa Mkoa wa Ruvuma kilichoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na kufanyika kwenye ukumbi wa SIDO  Mkoa wa Ruvuma mjini Songea.

Akizungumza wakati wa ufungaji wa kikao hicho. Katibu Tawala wa Mkoa Stephen Ndaki amewapongeza wafanyabiashara hao kwa kupitisha azimio hilo ambapo amewasisitizia kuwa maonesha hayo ni muhimu kwa kuwa yatapanua wigo wa biashara na kujenga mtandao utakaowapatia masoko endelevu.

Ndaki amesema serikali ya Mkoa wa Ruvuma ipo tayari  kuhakikisha kuwa Wazalishaji wa Bidhaa za Viwanda wanatumia kikamilifu fursa adhimu ya kushiriki katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda ili kupata teknolojia mpya .

“Soko ni vita,tusizalishe bidhaa na kukaa nazo,kwa hiyo tutoke kutafuta masoko ya bidhaa nje ya Mkoa  hivyo ni lazima tuwekeze na tutoke,lengo la serikali ni kuweka mazingira wezeshi ikiwemo kuongeza mitaji,Benki ya Kilimo tumezungumza nao wanakuja Ruvuma unaweza kuunganishwa nao’’,alisisitiza Ndaki.

Ndaki amesema Shirika la viwanda vidogo Tanzania SIDO nao wapo tayari kuongeza mitaji kwa wafanyabiashara ambao wanaweza kutoa mikopo hadi shilingi milioni 500.

Katibu Tawala huyo ametoa rai kwa maafisa biashara katika Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiriamali ili waweze kushiriki katika maonesho ya bidhaa za viwanda Desemba mwaka huu.

Norah Mishili ni Mwezeshaji kutoka TANTRADE  amelitaja lengo la Mamlaka hiyo ni kuona bidhaa zinazozalishwa nchini zinapata masoko yenye tija na njia  sahihi inayoweza  kukuza na kutangaza bidhaa za wazalishaji.

Amesema wakati wa Maonesho hayo washiriki watapata nafasi ya kujadili na kutatuliwa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika uzalishaji na kuwa na mazingira bora ya biashara.

Naye Afisa Biashara Mkoa wa Ruvuma Joseph Martin  ametoa rai kwa wajasirimali wadogo kwenda katika Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ili kupata mkopo isiyo na riba ambayo inatolewa kwa vijana,wanawake na wenye ulemavu.

Hata hivyo amesema  bidhaa za viwandani,zinahitaji soko  la ndani na nje ya Mkoa ambalo  linahitaji ushawishi  mkubwa hivyo  kuna umuhimu wa kushiriki Maonesho ya kimataifa ya bidhaa za viwanda ili kupanua wigo na kupata teknolojia mpya.

kauli mbiu ya ‘Nunua Bidhaa za Tanzania Jenga Tanzania’ inawapa nafasi wenye viwanda kutangaza bidhaa wanazozalisha na kuhamasisha matumizi ya bidhaa hizo kwa jamii nzima hivyo kupanua wigo wa masoko na kujenga uchumi wa nchi.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 18,2020

                                                             

 


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.