• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAFANYABIASHARA Ruvuma watakiwa kuuza mbolea kwa bei elekezi

Imewekwa kuanzia tarehe: September 6th, 2020

MKAGUZI wa Mbolea kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)Christian Mhando ,ametoa onyo kwa wafanyabiashara  wa mbolea kuhakikisha wanauza mbolea kwa bei elekezi kwa mbolea zote za kupandia na kukuzia.Katika Mkoa wa Ruvuma kuna kampuni saba za kununua mbolea na mawakala wa mbolea zaidi ya 120

Mhando ametoa onyo hilo wakati anakagua maghala ya kuhifadhia mbolea na mawakala wanauza mbolea katika maduka mbalimbali  mkoani Ruvuma.

“Wafanyabiashara hao wahakikishe wanatoa risiti za mashine mara baada ya kuuza mbolea hizo kwa wananchi,pia wauze mbolea ambazo zimesajiriwa na TFRA na kuzingatia utunzaji bora wa mbolea kwa kuwauzia wakulima mbolea zenye ubora,na yeyote atakayekwenda kinyume na maelekezo hayo atachukuliwa hatua’’,alisisitiza Mhando.

Mkaguzi huyo wa mbolea amewatahadhari wafanyabiashara kuacha tabia ya kuuza mifuko ya mbolea ambayo imefunguliwa ambapo anasema TFRA itachukua hatua Kali ikiwemo kuwanyang’anya leseni,kufunga biashara na kupelekwa mahakamani ili kufunguliwa mashitaka kwa mujibu wa sheria ya mbolea.

Hata hivyo amesema imebainika baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wanakiuka bei elekezi ya mbolea kwa kuongeza bei na kwamba changamoto hiyo imekuwa inajitokeza zaidi ya kwa wafanyabiashara wadogo ambapo amezipongeza kampuni za uuzaji wa mbolea kwa kuzingatia bei elekezi na kwamba baadhi ya Kampuni zimekuwa zinauza chini ya bei elekezi hivyo kuleta unafuu kwa wakulima.Mhando amesema kutokana na changamoto hizo kila mwaka wamekuwa wanakutana na wadau wa mbolea wakiwemo wawakilishi wa wakulima,wafanyabiashara wa mbolea na kampuni za mbolea ambapo wanapanga bei kwa pamoja na kuridhiwa na Waziri wa Kilimo kisha kutangaza bei elekezi.

Amesisitiza kuwa bei elekezi za mbolea za Tanzania zimekuwa rafiki kwa wakulima ukilinganisha na nchi nyingine hasa katika kipindi hiki cha janga la corona ambapo imebainika bei ya mbolea ya Tanzania ni ya chini zaidi hivyo kuleta unafuu kwa wakulima.

“Ukiangalia katika Mkoa wa Ruvuma katika msimu huu,mbolea ya kupandia bei yake haitazidi shilingi 50,000 kwa mfuko na mbolea ya kukuzia itakuwa kati ya shilingi 46,000 hadi 47,000 itategemea na mazingira ambayo mkulima yupo’’,alisema Mhando.

Mkaguzi huyo wa Mbolea wa TFRA  amesema serikali ya Awamu ya Tano inaendelea kujitahidi kuhakikisha kuwa bei ya mbolea kwa mkulima inaendelea kupungua na kwamba awali mfuko mmoja wa mbolea ulifikia zaidi ya shilingi laki moja ambapo hivi sasa imeshuka hadi kufikia chini ya shilingi 50,000.

Alisisitiza kuwa mbolea  ya Tanzania inauzwa kwa gharama nafuu hali inayosababisha wakati mwingine wafanyabiashara kutorosha mbolea hiyo kwenda kuuza katika nchi za jirani.

 Mhando anabainisha zaidi kuwa mbolea inapoingizwa nchini ,serikali ya  awamu ya Tano imeondoa tozo zaidi ya 114 ambazo zilikuwa zinaathiri wakulima hali ambayo imesababisha bei ya mbolea kuendelea kupungua.

Kwa upande wake Afisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Onesmo  Ngao ametoa rai kwa wakulima kuhakikisha wananunua mbolea yenye ubora na hasa katika kipindi hiki ambacho tayari serikali imetoa bei elekezi ya mbolea  katika Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla.

Ngao ameyataja mahitaji ya mbolea katika  katika Mkoa wa Ruvuma kwa msimu ujao wa 2020/2021  kuwa ni tani 50,000 na kwamba serikali inaendelea kuhimiza kampuni za  mbolea  kuingiza mbolea ambapo hadi sasa mbolea ambayo imeingizwa katika Mkoa wa Ruvuma ni zaidi ya  tani 3,500 na juhudi za kupeleka mbolea vijijini kwenye wakulima wengi zinaendelea.

Ametoa rai kwa wakulima mkoani Ruvuma katika kipindi hiki cha uuzaji wa mazao kununua mbolea kwa ajili ya matumizi ya msimu ujao wa kilimo ambapo hivi sasa maduka mengi yanauza mbolea chini ya bei elekezi.

 Katika msimu wa mwaka 2019/2020 Mkoa wa Ruvuma ulilima hekta 268,008 za mazao mbalimbali zilizotoa mavuno ya Tani 787,321 hii ni sawa na ongezeko la Tani 50,628.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Septemba 6,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.