• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAFANYABISHARA Ruvuma wafundishwa fursa zilizopo katika soko Huru la Afrika

Imewekwa kuanzia tarehe: August 30th, 2023

WAFANYABIASHARA wa Mkoa wa Ruvuma wamejengewa ufahamu kuhusu fursa zilizopo katika Soko huru la Afrika (AfCFTA) ili kupata uelewa na kuhamasika kutumia  soko huru la Afrika na kuuza bidhaa kutokea Tanzania.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea yameratibiwa na Taasisi ya Tan Trade iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara,na kufunguliwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Joel Mbewa.

Akizungumza kabla ya kufungua mafunzo hayo Katibu Tawala amelitaja lengo la mafunzo hayo kuwa ni mikakati ya kutumia fursa za kimasoko zilizopo katika eneo huru la biashara barani Afrika kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.

Amezitaja faida za mafunzo hayo kwa wafanyabiashara mkoani Ruvuma kuwa ni wafanya biashara kupata uelewa wa kutosha juu ya fursa  zinazopatikana katika sekta wanazofanyia kazi na kukua kwa idadi ya bidhaa zinazouzwa katika soko hilo kutokea Tanzania.

Faida nyingine za mafunzo hayo amezitaja kuwa ni kuboresha bidhaa zinazozalishwa ili kukabiliana na ushindani uliopo katika soko huru la Afrika,kuongezeka kwa bidhaa zinazozalishwa na kumiliki soko husika na kupata wanunuzi wa malighafi zilizopo mashambani kutokana na kuwepo kwa soko la kutosha.

“Ni Imani yangu mafunzo haya yatawajengea uelewa mkubwa katika kutumia fursa hizo ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla’’,alisisitiza.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo,Afisa Biashara Mkuu wa Taasisi ya TANTRADE Crispin Luanda amelitaja eneo la Biashara Huru la Bara la Afrika (AfCFTA) kuwa ndilo eneo kubwa zaidi la biashara huria duniani linaloleta Pamoja nchi 55 za Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya nane za kiuchumi za kikanda ili kuunda soko moja la bara la Afrika.

Hata hivyo amesema Tanzania ni Mwanachama rasmi wa AfCFTA toka mwaka 2021 ikiungana na nchi nyingine  za Soko Huru la Afrika.

Amezitaja nchi hizo kuwa ni Ghana, Kenya, Rwanda, Chad,Swaziland,Guinea,Mali,Namibia,Afrika ya Kusini, Jibouti, Mauritania, Uganda, Senegal, Kongo DRC,Togo, Misri, Ethiopia, Gambia, Sieraleone, Zimbabwe, Burkinafaso, Garbon, Equatorial Guineana Sao Tome.

Mtaalam huyo kutoka TANTRADE ametoa rai kwa wafanya biashara wa Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanatangaza biashara zao kwenye maonesho ya kimataifa kama Sabasaba ili kujitangaza kimataifa.

Awali wafanyabiashara hao waliipongeza serikali kwa kuboresha miundombinu ya barabara,majini na angani katika Mkoa wa Ruvuma hali ambayo inarahisisha utendaji kazi katika biashara zao.

Hata hivyo walizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni Pamoja na kuchelewa malipo ya bidhaa zao kama mazao,ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu biashara na changamoto ya leseni ya biashara.

Uongozi wa Mkoa wa Ruvuma na Taasisi ya TANTRADE imeahidi kuzitafutia ufumbuzi changamoto za wafanyabiashara ili waweze kufanya biashara zao kwa ufanisi  na kulifikia soko huru la Afrika kama ilivyo kwa wafanyabiashara katika nchi nyingine.

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.