Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imewapa mafunzo wahudumu wa afya kuhusu umuhimu wa lishe bora na uhusiano wake katika kuepuka udumavu na magonjwa yanayotokana na lishe duni. Mafunzo haya yameongozwa na Afisa Lishe Wilaya ya Tunduru Martini Kigosi.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru siku yalihusisha wauguzi, na wahudumu wengine wa afya.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Afisa Lishe Wilaya ya Tunduru Martini Kigosi ameeleza kuwa lishe bora ni msingi muhimu katika kuzuia magonjwa mengi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu, na utapiamlo.
Ameongeza kuwa wahudumu wa afya wanahitaji ujuzi wa kutosha kuhusu lishe ili waweze kutoa huduma bora na ushauri kwa wagonjwa wao na wananchi kiujumla hasa katika matibabu ya magonjwa yanayotokana na lishe duni.
Naye Leonatha Lutego, Maratibu huduma za afya ya Uzazi,Mama na Mtoto Wilayani Tunduru amesema wahudumu wa afya wanalo jukumu kubwa la kuwaelimisha wananchi kuhusu lishe bora na matumizi sahihi ya vyakula ili Kuondokana na tatizo udumavu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.