NAIBU Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Dkt Hashil T.Abdallah na Wajumbe wa kamati maalumu ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametembelea Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kujifunza.
Mkuu wa Msafara huo Katibu wa Wabunge wa CCM Rashidi shangazi mara baada ya kutembelea Kiwanda cha kukoboa Kahawa na vyama vya Ushirika katika Wilaya ya Mbinga na kuona swala zima la skabadhi ghalani amesema ni mfumo ambao unaongezea mazao thamani na kuleta tija kwa wakulima.
Mhe. Shangazi amesema kupitia mfumo wa Stakabadhi ghalani kuna maeneo ambayo yanachangamoto na inatakiwa kujifunza kwa wengine waliofanikiwa ili wajue hatua walizopitia na kufanikiwa na sera za kazi.
Amesema kwa wasimamizi wa Serikali lazima wajue changamoto na wazitatua ili waweze kufanikisha hata Ilani ya CCM imeamini mfumo huo unaweza kulifanikisha Taifa hasa katika mauzo ya nje kwa kuyaongezea thamani bila kuacha makampuni kujiendesha kiholela.
“Kama Taifa linaweza kuona fahari ya kujinasibu kuwa kuuza mazao nje mazao na kupelekea uchumi wa kati kwa kuwezesha viwanda vidogovidogo “
Shangazi ametoa wito kwa vikundi vya Ushirika na AMCOS kuwa na uaminifu ili wakulima wajiamini kuwa mfumo wa Stakabadhi ghalani ni mkombozi katika maisha yao.
Afisa mahusiano kutoka Bank ya NMB Amani Shabani amesema wamekuwa wadau wakubwa katika zao la Kahawa kwa Mkoa wa Ruvuma na wamefanikiwa kutoa mikopo mbalimbali kwaajili ya kuwezesha uzalishaji na ukusanyaji wa zao hilo.
Hata hivyo Shabani amesema mwaka 2019-2020 wametoa mikopo ya stakabadhi ghalani shilingi bilioni 9.2 mwaka 2020-2021 bilioni 11.4 na mikopo ya pembejeo milioni 900 pamoja na mwaka 2021-2022 mikopo ya stakabadhi ghalani bilioni 13.2 na pembejeo bilioni 2.8.
Amesema kwa msimu wa mwaka 2021-2022 wamefanikiwa kutoa mikopo ya pembejeo kwa vyama vya Ushirika 26 pamoja na wakulima 247 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.8.
Kwa upande wake Meneja wa chama cha Ushirika cha msingi Kimuli wamesema kimejikita katika miradi ya mazao,pembejeo,mashine za kusaga nafaka,mashamba ya miti,usafirishaji pamoja na maendeleo ya jamii na wameweza kufanikiwa kwa kujikwamua kimaisha na kijamii.
Amesema chama hicho kimeweza kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia fedha zilizotokana na mapato premium na ziada za ndani,kwa kukarabati majengo ya shule na Zahanati jumla ya zaidi ya shilingi milioni 229.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Septemba 24,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.