• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAKULIMA Ruvuma kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa mbegu bora

Imewekwa kuanzia tarehe: April 1st, 2023

CHANGAMOTO ya upatikanaji wa mbegu bora za mahindi kwa wakulima wa mikoa ya Ruvuma na Njombe,linakwenda kumalizika na kuwa Historia baada ya kampuni ya Zambia Seed Co Ltd kuanza kuzalisha mbegu  aina ZamSeed 638 katika shamba la Silverland Ndolela kata ya Mahanje Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma.

Akizungumza na wadau wa kilimo katika siku ya maonyesho ya mbinu bora za kilimo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Frank Kileo amesema,kuanzia msimu  wa kilimo 2023/2024 tatizo la upatikanaji wa mbegu linakwenda kuwa Historia kwa wakulima wa mikoa hiyo.

Alisema,mbegu za mahindi aina ya Zamseed 638 zitapatikana kwa wingi kwa mawakala  katika wilaya zote za mkoa wa Ruvuma na Njombe,na kuwataka wakulima kutembea kifua mbele kwa kuwa sasa wana uhakika wa kupata mbegu bora na kwa bei nafuu.

Kileo alisema,kampuni ya Zambia Seed C Ltd iko tayari wakati wote kutoa majibu ya changamoto za wakulima kuhusu ubora,upatikanaji na bei ya mbegu ndiyo maana imeamua kusogeza huduma zake mkoani Ruvuma.

Kwa mujibu wa Kileo,katika msimu 2022/2023 kulikuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa pembejeo hasa mbegu ambapo wafanyabiasahara walitumia nafasi hiyo kuuza mbegu kwa bei  ya juu.

Alisema, hali iliyosababisha baadhi ya wakulima kushindwa kumudu gharama na wengine kukata tamaa na hata kutoendelea na shughuli zao za kilimo,lakini uzalishaji wa mbegu ya Zamseed 638 unakwenda kutatua changamoto zote zilizojitokeza katika msimu huu wa kilimo.

Alisema,kampuni ya Zambia Seed Co Ltd itaendelea  kufanya tafiti mbalimbali wakati wote kwa kushirikiana na taasisi ya uthibiti wa ubora wa mbegu(TOSCI)ili kuhakikisha mbegu zinazozalishwa zinasajiliwa na kuwa na ubora ili kuongeza mavuno na kuwaondolea umaskini wakulima.

Kileo,amewashauri wakulima hapa nchini,kuanza kutumia mbegu zinazozalishwa na kampuni ya Zambia Seed Co Ltd ili kupata mavuno mengi,badala ya kutumia mbegu zinazozalishwa na makampuni mengine.

Amewaomba maafisa kilimo wa mikoa ya Ruvuma na Njombe na mikoa mbalimbali hapa nchini,kushirikiana na  kampuni hiyo katika kuunga mkono juhudi za  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika mkakati wake wa kuwainua wakulima kutoka katika umaskini.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Songea Wilman Ndile,amewataka wakulima kuzingatia kanuni za kilimo bora ili kupata tija katika shughuli zao za kilimo badala ya kuendelea na kilimo cha kizamani.

Alisema,kwa sasa kilimo ni biashara nzuri ambayo kama mkulima atafuata na kuzingatia kanuni za kilimo bora basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata mafanikio makubwa.

Alisema,kwa kutambua mchango na umuhimu wa wakulima kama kundi lenye mchango mkubwa kiuchumi hapa nchini, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeweka mfumo mzuri wa pembejeo za ruzuku zinazopatikana kwa bei nafuu.

Aidha Ndile,ameiomba kampuni hiyo kuuza mbegu zake kwa bei ndogo ili wakulima wengi waweze  kumudu na kutumia katika shughuli zao za kilimo na hakuna sababu ya kuuzwa kwa bei kubwa kwa kuwa inazalishwa mkoani Ruvuma.

Mkuu wa wilaya,amewatahadharisha wakulima wa mikoa hiyo kuepuka kununua mbegu za mitaani zisizokuwa na ubora wala kuthibitishwa na serikali kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea kupata mavuno kidogo licha ya jitihada  kubwa wanazofanya.

Baadhi ya wakulima, wameipongeza kampuni  hiyo kuanza kuzalisha mbegu bora za mahindi ambazo zinakwenda kuongeza hamasa  na kuchochea uzalishaji wa mazao mashambani.

Gelodian Millinga alisema,mafunzo hayo yatawasaidia wakulima kuongeza uzalishaji hasa kuanzia uandaaji wa shamba,upandaji na wakati wa kuweka mbolea.

Wilbroad Nyoni alisema, katika shughuli zao za kilimo changamoto kubwa ilikuwa upatikanaji wa mbegu bora kwani baadhi ya mawakala wasiokuwa waaminifu wanauza pembejeo zilizopita muda wa matumizi kutokana na tamaa ya fedha bila kujali upande wa wakulima.

Alisema,ujio wa kampuni hiyo na kuanza kuzalishwa kwa mbegu za mahindi aina ya Zamseed 638 katika mkoa wa Ruvuma,ni faraja kubwa kwa wakulima ambao sasa wana matumaini ya kupata pembejeo bora na bei nafuu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.