WAKULIMA Ruvuma wamenufaika na mfumo wa Mazao Stakabadhi Ghalani kwa misimu mitatu mfululizo kwa mazao ya Ufuta,Mbaazi,Soya, Korosho na Kahawa kwa zaidi ya Shilingi bilioni 283.
Akitoa taarifa hiyo Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Jeremia Sendoro amesema uendeshaji wa mazao ya Ufuta,Soya pamoja na Mbaazi umefanyika kupitia wakulima kukusanya mazao kupitia vyama vya msingi 88 na vyama vikuu .
Amesema kwa msimu wa mwaka 2020/2021 jumla ya minada 29 ya ufuta ilifanyika ambapo jumla kilo 8,326,686 za ufuta ziliuzwa kwa bei ya juu sh.2,393 na bei ya chini 1,998 na kuwapatia wakulima zaidi ya shilingi milioni 17,na kwa kipindi cha msimu wa mwaka 2018/2019 hadi 2021 Julai Mkoa wa Ruvuma ulukusanya kilo za ufuta 28,989,711 na kuuza kwa bei ya sh2,393 wakulima walipata zaidi ya shilingi bilioni 69.
Hata hivyo Sendoro amesema kwa msimu wa kilimo cha 2018/2019 hadi 2021 Julai jumla ya kilo za Soya zilikusanywa kwa wastani wa kilo 4,963,088 wakulima walijipatia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 5.
Amesema kwa zao la Mbaazi mwaka 2018/2019 hadi 2021 Septemba walikusanya wastani wa kilo 12,165,680 wakulima walijipatia zaidi ya shilingi bilioni 12,Korosho mwaka 2017/2018 hadi kufikia mwaka 2020/2021 walikusanya kilo 79,535,246 na wakulima walipata zaidi ya shilingi bilioni 241 pamoja na zao la Kahawa mwaka 2017/2018 hadi kufikia msimu wa mwaka 2020/2021 jumla ya kilo 63,908,344 kahawa zilikusanywa na kuuzwa kwa bei 4,000 wakulima walijipatia zaidi ya shilingi bilioni 255.
Akizungumzia mafanikio ya mfumo wa stakabadhi ghalaniSendoro amesema ikiwemo wakulima kupata bei nzuri hususani mzao yanayouzwa katika mfumo huo,kuwepo kwa ushirikiano mzuri kwa wadau,kuwepo kwa matumizi sahihi ya vipimo,kupunguza kiasi cha utoroshwaji,pamoja na mapato ya Halmashauri.
Katibu tawala msaidizi amesema changamoto za mfumo huo baadhi ya madalali kuwashawishi na kuwarubuni wakulima,Uelewa wa mfumo huo bado upo chini hususani Halmashauri ya Madaba na Nyasa upo chini,Hali ya mazao bado upo chini kitija pamoja na kuto pima hali ya afya ya udongo.
Sendoro ameeleza mpango mkakati wa kukabiliana na changamoto hizo kuwa Mkoa wa Ruvuma umejipanga kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuwa umeleta auheni kwa wakulima,Mkoa umeendelea kusimamia maelekezo ya Serikali Maafisa ugani waelekeze majukumu yao na wasimamie ipasavyo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema kapitia mfumo wa stakabadhi ghalani siyo kuboresha mfumo bali kuanzia mbegu bora ili Mkoa wa Ruvuma uwe na kilimo cha tija zaidi na uwezo wa kuandaa mashamba kabla ya kulima .
“Tumejipanga kuanza kilimo cha mazao ya biashara kikubwa zaidi cha kimkakati ikiwemo grobal farming kinavyoelekeza hata ilani ya CCM inaelekeza”.
Hata hivyo Ibuge amekaribisha kilimo cha mkataba katika Mkoa huo na kitakuwa cha bei nzuri wakati wa mavuno ni fursa kwa wakulima na kuendelea kuimarisha Ushirika.
Amesema mfumo wa stakabadhi ghalani unamhakikishi mkulima usalama katika kuuzao mazao yake na amewasihi viongozi wanaosimamia vyama vya msingi kuwa wazalendo nakuto wapunja wakulima ili waendelee kunufaika na mfumo huo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Septemba 27,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.