WAKULIMA mkoani Ruvuma wameshauri kutumia trekta dogo rafiki wa mkulima ambalo linatumia mafuta lita mbili kulima hekari moja kwa dakika 30.
Ushauri huo umetolewa katika maonesho ya nanenane mkoa wa Ruvuma na Venance Komba Afisa Masoko wa Kampuni ya ATC AGRO inayojishughulisha na uuzaji wa matrekta madogo ambayo yanauzwa kwa gharama nafuu
Komba amesema trekta hilo dogo linarahisisha kilimo na kwamba trekta hilo linapatikana kwa gharama nafuu na rahisi kwacsababu siyo watu wengi wana uwezo wa kununua trekta kubwa ya milioni 60 .
‘’Trekta hili ndogo linatumia gharama kidogo na kutoa matokea makubwa ,linatumia mafuta lita 2 kwa hekari,service yake ni ndogo unamwaga oil lita 10 kwenye gia boksi, ni nafuu kwa matumizi ya mkulima mdogo’’,alisisitiza.
Komba amesema kwa Mkoa wa Ruvuma na mikoa mingine ya kusini trekta hilo linapatikana kwa gharama ya shilingi milioni 27 .
Afisa masoko amesema kampuni yao imeingia mkataba na Benki ya CRDB na kwamba Matrekta hayo yanapatikana kwa Mkopo au kulipa fedha taslimu.
Maonesho ya Nane nane hufanyika kila mwaka hapa nchini ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni. ’kwa maendeleo ya kilimo,mifugo na uvuvi chagua viongozi bora 2020’’,kaulimbiu hii imelenga kuwasisitiza wananchi wote kushiriki katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 2020.
Imeandikwa NA Anet Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Agosti 8,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.