WAKULIMA wa Mbaazi Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wameingiza zaidi ya shilingi bilioni 1.69 baada ya kuuza Kilo 839,940 za mbaazi katika Mnada wa kwanza Msimu wa mwaka 2022/2023.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Oparesheni wa Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU) Bw. Marcelino Mrope wakati akizungumza na Wanahabari ofisini kwake Mjini Tunduru.
Bw, Mrope amesema TAMCU katika msimu wa Mwaka 2023/2024 imejiwekea malengo ya kukusanya Mbaazi Kilo 5,350,788 na kwamba katika msimu huu Chama kimeagiza viroba 130,000 kwa ajili ya kuhifadhia Mbaazi.
Hata hivyo, amesema kuwa ukusanyaji wa Mbaazi katika msimu wa 2022/2023 uliendelea kuuzwa kwa mfumo wa Stakabadhi Ghalani, ambapo jumla ya Minada sita ilifanyika na Kilo 3, 035,692 ziliuzwa na kuwaingizia Wakulima zaidi shilingi bilioni 2.6.
“ukusanyaji wa zao la Mbaazi umepungua kidogo kutoka kilo 4,111,845 msimu wa mwaka 2021/2022 hadi kilo 3,035,692 msimu wa mwaka 2022/2023 ambapo ni sawa na anguko la asilimia 26.17 la ukusanyaji katika mauzo”, alisema.
Mnada wa pili wa zao la mbaazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru unatarajia kufanyika Agosti 24,2023
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.