WAKULIMA wa mahindi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma,wameitaja changamoto ya kukosa elimu ya matumizi sahihi ya pembejeo ikiwemo mbegu bora na mbolea kutoka kwa maafisa ugani hali iliyosababisha kuzalisha mazao yasiyo kidhi viwango kulingana na mahitaji ya soko la Serikali.
Wamesema hayo,wakati wa kazi ya uuzaji na ununuzi wa zao la mahindi unaofanywa na Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula(NFRA) katika kituo cha Rwinga wilayani humo.
Faraji Abed amesema,wakulima wako tayari kuzalisha,lakini elimu ya uzalishaji wa mazao bora ni kikwazo kikubwa ambacho kimesababisha baadhi ya wakulima kukata tamaa na kushindwa kuendelea na uzalishaji mashambani.
“tunaiomba Serikali maafisa ugani tuwe nao mashambani ili sisi wakulima tusiendelee kupata hasara ya kuchagua mazao yetu pindi tunapofikisha sokoni,kama maafisa kilimo tungekuwa nao kuanzia wakati wa maandalizi ya shamba hadi msimu wa mavuno basi tusingepata hasara kubwa namna hii”alisema Abed.
Amesema,wakulima wana mwamko mkubwa wa kulima,lakini changamoto kubwa ni kupata mazao yenye sifa ya kufikisha sokoni yakiwa na ubora wake ule ule hali inayopelekea wakulima kuamini kama kilimo ni kazi inayoweza kuwaletea manufaa katika maisha yao.
Ameishukuru serikali kwa kununua mahindi kwa bei ya Shilingi 700 kwa kilo moja ikilinganisha na bei ya Shilingi 350 ya wafanyabiashara wa mitaani ambayo haikidhi mahitaji na gharama za uzalishaji.
Mkazi wa kijiji cha Rwinga Salum Idd,ameishukuru Serikali kuwaletea kituo cha ununuzi wa mahindi,lakini changamoto kubwa wanatumia muda mrefu kusafisha mahindi kabla ya kupokelewa.
Amesema,hali hiyo imetokana na uzembe wa maafisa ugani ambao hawakwenda mashambani kuwapa elimu ya kilimo cha kisasa hasa katika matumizi ya mbegu bora na mbolea.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.