• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAKULIMA wa ufuta Tunduru waendelea kuvuna fedha,wapongeza mfumo wa stakabadhi ghalani

Imewekwa kuanzia tarehe: July 11th, 2022

WAKULIMA wa ufuta wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,wamezidi kuvuna fedha kufuatia bei ya zao hilo kupanda kutoka Sh.3,022 kwa kilo moja katika mnada wa pili  hadi Sh.3,095 katika mnada wa tatu uliofanyika katika Chama cha msingi cha Ushirika Mluji(Amcos) kijiji cha Mchesi.

Meneja masoko wa Chama kikuu cha Ushirika wilayani Tunduru(Tamcu Ltd) Marcelino Mrope alisema,katika mnada wa tatu jumla ya kilo 670,040 zenye thamani ya Sh.bilioni 2,073,773.800 zimekusanywa na kuuzwa  kwa mfumo wa stakabadhi ghalani na wakulima wanaohudumiwa na Chama chama hicho.

Aidha alisema, katika mnada wa kwanza jumla ya kilo,1,008,638 zenye thamani ya Sh.bilioni 3,008,700.143 ziliuzwa kwa wastani wa bei ya Sh.2,982.93 na katika mnada wa pili kilo 507,522 zenye thamani ya Sh.bilioni 1,533,916,440.00 ziliuzwa kwa bei ya Sh.3,022 kwa kilo moja.

Alisema,katika minada miwili ya awali jumla ya ufuta uliouzwa ni kilo 1,516,160 zenye thamani ya Sh.bilioni 4.5 kati ya fedha hizo bilioni 4.4 zimekwenda kwa wakulima pamoja na watoa huduma ambao ni wasafirishaji.

Akifunga mnada huo Mwenyekiti wa Tamcu Mussa Manjaule alisema, jumla ya makampuni tisa yalijitokeza katika mnada huo,lakini ni makampuni matatu tu ya Export Trading,Yuri Investment na Rv Export yaliyokubaliwa kununua ufuta katika mnada wa tatu.

Manjaule,amewapongeza wakulima kwa kukubali kuuza ufuta wao kwa bei nzuri na kuwataka kuongeza kasi ya uzalishaji katika msimu ujao.

“wakulima wa wilaya ya Tunduru wanaishukuru sana serikali kwa kufanya maamuzi ya kuwakomboa wakulima wake kwa kuuza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umeendelea kuwa na manufaa makubwa kwa wakulima”alisema.

Alisema,serikali imefanya maamuzi sahihi kuanzisha minada ya ufuta na baadhi ya mazao na hayo ni mfanikio  na ukombozi mkubwa wa kiuchumi kwa wakulima wa wilaya ya Tunduru.

Manjaule,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan  kutoa pembejeo  kwa wakulima wa korosho bure,hata hivyo amewakumbusha wakulima kujiwekea akiba ya fedha wanazopata  kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa zao la korosho, badala ya kuzitumia fedha  hizo kwenye mambo yasiofaa ikiwamo ulevi.

Manjaule ambaye ni mjumbe wa bodi ya KoroshoTanzania,amewakumbusha wakulima kulipa madeni  yote wanayodaiwa na taasisi za fedha ili wawe na sifa ya kukopesheka kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za kilimo.

Amewataka kufungua akaunti kwa ajili ya kuingiziwa malipo yao,badala ya kutumia akaunti za watu wengine ambao baadhi sio waaminifu ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Kwa upande wake Afisa Ushirika wa wilaya ya Tunduru George Bisani alisema, katika msimu wa mwaka huu uzalishaji wa zao la ufuta sio mkubwa kutokana na wakulima wengi kujikita sana kwenye zao la Alizeti na mbaazi.

Bisani,amewaomba wakulima wa Tarafa ya Lukumbule kuongeza ukubwa wa mashamba yao na kulima mazao mchanganyiko  ili kujiongezea kipato, badala ya kujikita kwenye zao moja tu la Korosho au Ufuta.

Amewaasa,kuendelea na utaratibu wa kuuza ufuta na mazao mengine kwa mfumo wa stakabadhi ghalani,kwani tangu ulipoanzishwa umekuwa na manufaa makubwa si kwa wakulima wenyewe bali hata kwa wafanyabiashara na Serikali kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wengine Yusufu Twaha,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuimarisha  mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umewasaidia sana wakulima kuwa na uhakika wa soko na kupata bei nzuri.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.