MKOA wa Ruvuma umenufaika na Mbegu bora za Mahindi aina ya DKC 9089 tani 25 zenye thamani ya shilingi Milioni miamoja hamsini kutoka kampuni ya Baya kupitia shirika lisilo la kiserikali ( ACT) Balaza la kilimo.
Akitoa taarifa hiyo Afisa kilimo Mwandamizi wa Mkoa wa Ruvuma Enock Ndunguru amesema Msaada wa Mbegu umetolewa kwa Nchi nzima kwaajili ya kusaidia wakulima wadogo kupitia ugonjwa wa Corona kwa Mkoa wa Ruvuma tani hizo 25 zimenufaisha Halmashauri 2,Mbinga vijijini na Songea vijijini.
Ndunguru amesema Mbegu hizo zimegawiwa kwa wananchi zaidi ya Elfu nane,elfu nne kutoka Halmashauri ya Mbinga na Elfu nne kutoka Halmashauri ya Songea Vijijini na wanufaika wamepata Mbegu za kutosha kwa robo heka yani kilo 2 mpaka nusu heka kilo 4.
“Hizi mbegu zote zinatolewa bure haziuzwi na muundo wa kuwapata wakulima wadogo umeelekezwa kwa wakulima wadogo,Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga na Songea na wakuu wa idara za Kilimo na Mabwana shamba ndio walioshirikiana na watendaji wa vijiji kupata orodha ya wanufaika”.
Hata hivyo afisa kilimo mwandambizi wa Mkoa akielezea Mbegu hizo aina ya DKC 9089 amesema zinauwezo wa kuzaa gunia 40 kwa hekari hadi 44 Mbegu zimekwisha kufika na wamekwisha sambaza kwa Halmashauri husika na kuwafikia wanufaika zaidi ya elfu nane
Ndunguru amesema Shirika ACT limeanza kufanya kazi kwa Mkoa wa Ruvuma kuanzia mwaka 2000 kwa kuwajengea wakulima uwezo wa kulima kilimo bora na kilimo kinaleta tija kwa wakulima.
Hata hivyo shirika hilo litaendelea kusimamia kwa karibu kwa maeneo ambayo mbegu imeenda Wilaya ya Mbinga vijijini na Wilaya ya Songea Vijijini.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Halmashauri ya Madaba
JANUARI 4,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.