UTEKELEZAJI wa Mpango wa TASAF Mkoa wa Ruvuma umesaidia walengwa 19,216 wamejiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (ICHF).
Akizungumza Mratibu wa TASAF Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira amesema ongezeko la fursa za Afya walengwa wanaoishi maeneo ya vijijini wanahimizwa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (ICHF),wanaoishi Mjini wanahimizwa kujiunga na Mfuko wa Tiba kwa kadi (TIKA).
Mratibu amesema hadi kufikia Juni,2022 jumla ya walengwa 19,216 wamejiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ikiwa sawa na asilimia 29.1.
Mlimira ametaja mafanikio ya TASAF ikiwemo asilimia 99 ya walengwa wanatimiza masharti ya Elimu na afya,walengwa 19,216 wanaoishi maeneo ya vijijini na mjini wamehamasika kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) ikiwa uhamasishaji unaendelea.
Amesema kipindi cha Julai hadi Juni Mkoa wa Ruvuma ulipokea magari 5 katika Halmashauri 5 kwaajili ya utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya maskini.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 6,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.