Ofisi ya Rais TAMISEMI, kupitia Mradi wa BOOST, imetoa mafunzo kwa walimu wakuu 64 na walimu wanaofundisha shule za awali katika shule za msingi 64, jumla ikiwa walimu 128. Mafunzo hayo yanalenga kuboresha elimu ya awali kwa kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma, kuandika, na kuhesabu.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Nyasa, iliyopo katika kijiji cha Kilosa, kata ya Kilosa, wilayani Nyasa.
Mratibu wa mafunzo hayo, Mwalimu Godfried Mapunda, amesema lengo kuu ni kuwajengea uwezo walimu ili waweze kufundisha wanafunzi kwa ufanisi zaidi kwa kutumia zana bora za kujifunzia. Hii itasaidia wanafunzi kupenda shule na kupata maarifa ya msingi kwa ubora.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.