• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WALIMU 600 kuajiriwa na mradi wa GPE

Imewekwa kuanzia tarehe: March 1st, 2024

Mradi wa  Global Partnership for Education (GPE) utaongeza fursa ya upatikanaji wa Elimu bora kwa watoto kuanzia ngazi  ya Elimu ya Awali, Msingi, Elimu maalum na Elimu kwa walio katika mfumo usio rasmi hususan wanaotoka katika mazingira hatarishi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankhoo wakati akifungua kikao cha (GPE) kilichofanyika katika Ukumbi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa,Songea.

Serikali kupitia mradi huo inatarajia kuajiri walimu wa kujitolea  600 ambao watalipwa kila mwezi shilingi laki tatu na kwamba mradi huo wa miaka miwili unatekelezwa  kwa ufadhili wa shilingi bilioni 212.

Mwankhoo amesema kupitia mradi huo serikali  itaboresha mazingira ya walimu kwa kujenga nyumba za walimu katika maeneo ya pembezoni  na kuwahamasisha walimu kwa kuwapa motisha 

“Mradi wa GPE unatoa ufadhili wa masomo kwa walimu wanaofundisha elimu maalumu ili kuwajengea uwezo mkubwa zaidi katika kazi”, amesema Mwankhoo.

Amelitaja lengo la mradi huu kuwa  ni kuimarisha mfumo wa motisha kwa walimu wanaofundisha shule za pembezoni na kutekeleza mpango wa ajira kwa walimu wa kujitolea ambapo zaidi ya walimu 600 wataingizwa katika mradi huo na kupewa posho ya shilingi laki  tatu kwa mwezi.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dionice Lukweme amesema mradi huo umekuja na mfumo ambao utawezesha kuwasimamia walimu watakaokuwa wanajitolea katika shule.

Amesisitiza kuwa  kupitia mfumo huo  watakuwa na takwimu ya walimu wote wanao jitolea katika shule zote nchini.

Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Eva Mosha amesema mradi unatengeneza mazingira rafiki  ya kufundisha na kujifunza Kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na walimu,

 Amebainisha zaidi kuwa mradi huo  unafadhiliwa kwa Dola za Marekani milioni 84 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 212 ambapo amekitaja  kipaumbele cha kwanza ni kujenga nyumba za walimu katika Halmashauri ambazo zipo pembezoni.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mfaranyaki Zuhura Nikata amesema mradi huu utatatua changamoto za walimu kwa asilimia 90 kwa kuwa utawajengea  walimu makazi jirani na vituo vyao vya kazi na kutoa posho kwa walimu wanaojitolea Kwa muda wa miaka miwili.

Kwa upande wake Mwalimu wa Shule ya Msingi Amani, Ayubu Ng'ombo Yahaya amesema mradi huu utawasaidia walimu kupata mbinu mpya za  kufundishia na kuhamia katika mfumo wa kisasa wa kijiditali.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.