WALIMU wa shule za msingi na Sekondari katika Halmashauri ya wilaya Mbinga,wamefanya mabonanza ya michezo ili kuimarisha afya zao,na kupata mbinu zitakazo saidia wanafunzi wao kufanya vizuri wanaposhiriki michezo mbalimbali.
Mabonanza hayo yanayofahamika Sabina Lipukila KUT CWT Cup 2022-2023,yamefanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Kihamili kata ya Kigonsera wilayani Mbinga.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo mdhamini Mkuu wa michezo hiyo Sabina Lipukila alisema,michezo hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapa mbinu mbalimbali walimu katika kufundisha michezo wanafunzi wa mkoa wa Ruvuma na kuondokana na kufanya vibaya katika mashindano ya shule za msingi(Umitashumta) na Sekondari(Umisseta).
Aidha alisema,kupitia mabonanza hayo walimu watakutana,kufahamiana na kuwa na hali ya kushiriki katika michezo ambayo itaongeza hisia ya mafanikio na uzalendo katika majukumu yao ya kila siku.
Amewapongeza walimu wa Halmashauri ya wilaya Mbinga, kwa kushiriki bonanza hilo ambalo linakwenda kusaidia kuibua vipaji na hatimaye kupata wanamichezo bora watakao iwakilisha wilaya ya Mbinga na mkoa wa Ruvuma kwenye mashindano mbalimbali.
Lipukila ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) kutoka mkoa wa Ruvuma alisema, CWT kinatambua sana umuhimu wa michezo ambapo kwa nyakati tofauti walimu wamepata nafasi ya kushiriki michezo ndani na nje ya nchi.
Amehaidi kuendelea kudhamini michezo kwa wanafunzi na walimu wa shule za msingi na sekondari ili na kuwaomba wadau wengine kusaidia kudhamini katika sekta ya michezo ambayo imeanza kuleta manufaa makubwa kwa wana michezo na Taifa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu wilaya ya Mbinga Ahmad Mwalimu amesema, katika kuunga mkono michezo Chama hicho kitatoa seti moja ya jezi kwa kila timu.
Baadhi ya walimu,wamempongeza mdhamini wa bonanza hilo Sabina Lipukila kwa kuamua kuanzisha mabonanza ya michezo ambayo yatasaidia kuibua vipaji vingi na kuimarisha afya za walimu.
Katika Bonanza hilo Timu ya walimu ya mpira wa miguu kutoka Bonde la Hagati imeibuka mshindi baada ya kuifunga Timu ya kanda ya Kigonsera kwa Penati 5-3 huku timu ya Netball wanawake ya Walimu ikiifunga timu ya Halmashauri ya wilaya Mbinga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.