Afisa Elimu Awali na Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Saada Chwaya, amefungua mafunzo ya walimu wa elimu ya awali yanayofanyika kwa siku nne chini ya mradi wa BOOST.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Chwaya alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuboresha ufundishaji wa elimu ya awali, hatua inayochangia kuboresha msingi wa elimu nchini. Alifananisha hatua hiyo na ujenzi wa nyumba, akisisitiza kuwa msingi imara huwezesha maendeleo mazuri ya mwanafunzi kuanzia darasa la awali.
“Msingi ukiwa imara, mwanafunzi hatakuwa na changamoto atakapofika darasa la kwanza. Serikali imedhamiria kuboresha elimu kuanzia ngazi ya Taifa hadi Wilaya. Baada ya mafunzo haya, ni jukumu letu walimu kuhakikisha tunatekeleza kwa vitendo yale tuliyojifunza,” alisema Chwaya.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa mafunzo hayo kutoa matokeo chanya ili kukidhi matarajio ya Serikali. Alisema wakaguzi wa elimu wanatarajiwa kuthibitisha kuwa walimu wamepata ujuzi unaohitajika na wanafanya kazi kwa weledi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.