MAAFISA Elimu na Walimu wa Elimu Maalumu 56 wamepatiwa mafunzo ya Elimu Jumuishi kwa muda wa siku tatu mkoani Ruvuma.
Akifunga mafunzo hayo Mkurugenzi wa Elimu Maalumu TAMISEMI Juliasi Migeha amesema Mafunzo hayo yanafanyika katika Mikoa ya Morogoro,Iringa ,Mtwara na Ruvuma ili kuwezesha maafisa na walimu wa elimu maalum kufanya kazi kwa viwango.
Mkurugenzi huyo amezitaja changamoto za watoto wenye mahitaji maalumu kuwa ni kutengwa na kuwaweka katika madarasa maalum wakati wanafundishwa ikiwa wakitoka.
Migeha amesema watoto hao wanapaswa kukua na kujifunza kwa pamoja kupitia walimu jumuishi wa kuwafundisha na kuwawekea mikakati ya kuwawezesha kufanya vizuri katika masomo yao.
Hata hivyo Migeha ametoa rai kwa walimu hao kuwa na Mkakati wa utekelezaji wa Elimu Jumuishi katika mfumo mzuri na kwamba kila Halmashauri iweze kutambua idadi ya watoto wenye uhitaji maalumu ili wanapoanza masomo yao wasipate changamoto za kukosa kujiunga na Masomo kwa wakati.
“Changamoto ya Elimu Jumuishi ni miundombinu kuto kuwa rafiki,vifaa,walimu wenye uwezo wa kufundisha na kuwafanya wanafunzi kuelewe “,alisema.
Kwa pande wake Katibu Tawala Msaidizi Elimu Mkoa wa Ruvuma Imanuel Kisongo kupitia mafunzo hayo amewaasa Maafisa na walimu wa elimu maalum kutoa matunda kupitia mafunzo ya elimu jumuishi.
Kisongo ameahidi kutembelea shule zote za elimu maalum katika Mkoa huo kujua changamoto zake na amewaomba maafisa na walimu wa elimu maalum kujituma kutokana na kazi ambayo wamepewa pamoja na kutoa Taarifa kwa wakati ili kuhakikisha wanafunzi wanapata Elimu iliyo sahihi.
Mmoja kati ya washiriki kutoka katika Shule ya St Vicent Ruhuwiko Manispaa ya Songea Sister Agneta Mlelwa amesema kupitia mafunzo ya Elimu Jumuishi yatawawezesha kuwafundisha wanafunzi wa aina zote wenye ulemavu na wasiokuwa na ulemavu.
Mlelwa ameiomba Serikali kutoa mafunzo hayo mara kwa mara sanjari na vifaa vya kufundishia ili kutoa elimu bora.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kitengo cha Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Machi 10,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.