Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Simon Kemori Chacha amewataka walimu wakuu na walimu wa michezo mashuleni kuhakikisha kuwa ratiba ya michezo zinazingatiwa na wanafunzi wapewe nafasi ya kushiriki michezo na sanaa katika shule zote za Msingi na Sekondari.
Ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya ugawaji wa mipira kwa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Mkuu wa Wilaya amewataka walimu pia kuhamasisha wanafunzi kushiriki katika michezo mingine kama vile riadha, mpira wa kikapu, na netiboli.
Amesisitiza kuwa michezo ni muhimu kwa afya ya mwili na akili ya wanafunzi, na pia inawasaidia kukuza nidhamu na ushiriki
“tunatakiwa kuhakikisha vifaa hivi tunavitunza na kutumika kwa usahihi kama lengo la Serikali yetu katika kukuza michezo”. Alisema DC Chacha.
Afisa Michezo wa Halmashuri ya Wilaya Tunduru, Abilahi Namkopo, ameelezea Mipira hiyo ni zao la utekelezaji wa mpango wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) unaoitwa "Football for Schools" na kwamba Mpango huo unalenga kukuza vipaji vya vijana wenye umri kuanzia miaka 8 hadi 17, wengi wao wanapatikana shuleni.
Jumla ya mipira 92 imegawiwa kwa shule sita za msingi na sekondari wilayani Tunduru.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.