• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANAFUNZI 800 wafanya utalii wa ndani hifadhi ya asili Ruhila Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: September 7th, 2023

WANAFUNZI 800 wa shule mbalimbali wilayani Songea mkoani Ruvuma wametembelea bustani ya wanyamapori ya Ruhila iliyopo mjini Songea mkoani Ruvuma kwa lengo la kufanya utalii wa ndani.

Afisa Utalii wa Bustani ya asili Ruhila ambayo ipo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) David Tesha amesema wanafunzi hao walifika kutalii katika bustani hiyo katika kipindi cha kunzia Julai hadi Agosti mwaka huu.

“Maafisa uhifadhi wa Bustani ya Ruhila wamekuwa wanapita katika shule za msingi na sekondari mkoani Ruvuma kwa lengo la kutoa elimu ya utalii na uhifadhi,hali hiyo imechangia idadi kubwa ya wanafunzi kila mwezi kutembelea bustani yetu ya Ruhila’’.alisisitiza Tesha.

Amesema wanafunzi hao wakiwa katika bustani hiyo wameweza kutalii na kujifunza mambo mbalimbali ya uhifadhi na utalii Pamoja na kufurahia michezo ya kuendesha baskeli na michezo ya kubembea.

Hata hivyo amesema katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2023 zaidi ya watalii 3,420 kutoka ndani na nje ya nchi wameweza kutembelea katika bustani ya Ruhila.

Amewataja watalii kutoka nje ya nchi  ambao wametembelea katika bustani hiyo kuwa wanatoka katika nchi za Japan, Sweden,Norway,Nchi za Kiarabu,Nchi za Sikandinavia na Kenya na  ametoa rai kwa watanzania kujenga utamaduni wa kufanya utalii wa ndani kwa  kutembelea vivutio vya utalii  kama bustani ya wanyamapori Ruhila ambayo ipo mjini Songea.

Amewataja Wanyama ambao wanapatikana katika bustani hiyo kuwa ni simba,pundamilia, pofu, kakakuona, kuro, swalapala, sungura, nyumbu,jamii ya nyani ambapo amesema bustani hiyo ina madhari ya kuvutia yakiwemo maeneo mazuri ya kupigia picha na kuweka kambi kwa ajili ya utafiti

Bustani ya asili ya Ruhila ambayo ipo chini ya TAWA ilianzishwa mwaka 1973 na imekuwa inapokea watalii wa aina mbalimbali kutoka ndani ya nje ya nchi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.