Maafisa kutoka Kitengo cha Ustawi wa Jamii, Idara ya Maendeleo ya Jamii, na Dawati la Jinsia na Watoto katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wamewapa wanafunzi elimu kuhusu jinsia, haki za mtoto, na makatazo ya kisheria.
Elimu hiyo ilitolewa kwa wanafunzi wa shule tatu za sekondari katika Halmashauri hiyo ambazo ni Shule ya Sekondari Matemanga, Shule ya Sekondari Kiuma, na Shule ya Sekondari Namwinyu.
Mtaalamu kutoka Jeshi la Polisi, Koplo Humphrey, alieleza kuhusu masuala ya kijinsia na sheria, akiwahimiza wanafunzi kutambua na kuzuia aina zote za ukatili na unyanyasaji.
Baada ya mafunzo hayo, wanafunzi wa kike walipokea sodo/pedi kutoka kwa taasisi ya PAMS FOUNDATION pamoja na elimu ya hedhi salama ili kuwawezesha kuhudhuria masomo bila vikwazo.
Juhudi hizi zinalenga kuwaelimisha na kuwalinda wanafunzi dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuwajengea uelewa wa haki zao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.