Wanafunzi 76,962 kutoka shule 102 katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, wanatarajiwa kupatiwa dawa za kinga dhidi ya magonjwa ya minyoo ya tumbo na kichocho.
Zoezi hilo kinafanyika kwa siku mbili, kuanzia tarehe Januari 23 hadi 24 2025, likiwalenga watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 14.
Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Mratibu wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele katika Manispaa hiyo, Dr.Bload Komba, amewahakikishia wazazi kuwa dawa hizo ni salama kwa matumizi na zinalenga kuimarisha afya ya watoto dhidi ya magonjwa hayo.
Mratibu huyo amewataka wazazi na walezi kushirikiana na kuhakikisha watoto wote walengwa wanahudhuria ili kupata kinga hiyo muhimu kwa afya yao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.