WANANCHI wa Mtaa wa Masasi na Lusewa kata ya Luhuwiko Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma wameibua mradi wa ujenzi wa shule ili kuwawezesha Watoto wao kupata elimu eneo la Jirani.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini Mhe Jonas Mbunda ameahidi kutoa vifaa mbalimbali vya umaliziaji wa ujenzi wa shule ya Msingi Lusewa.
Vifaa ambavyo Mbunge huyo ameahidi kutoa ni matofali 500 kwa ajili ya ujenzi wa matundu vyoo, mifuko 30 ya saruji na fedha kiasi cha shilingi laki tano.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi huo , Afisa MtendajI Mtaa wa Masasi Kasmir komba amesema ujenzi wa shule ya Msingi Lusewa ulianza kujengwa Desemba 29,2022 ikiwa na lengo la kujenga vyumba tisa vya madarasa na ofisi nne ambapo hadi sasa wameanza na ujenzi wa vyumba vitatu na ofisi moja vilivyogharimu shilingi milioni 60.
Amesema wananchi wa kata hizo waliamua kuibua mradi wa ujenzi wa shule, baada ya kuwepo kwa changamoto ya umbali mrefu wa watoto wao kufuata shule.
Hata hivyo ili kuhakikisha mradi unatekelezwa wananchi wamekubaliana kila kaya kuchangia shilingi 250,000.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.