• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANANCHI Ruvuma wanavyomuunga mkono Rais Samia

Imewekwa kuanzia tarehe: October 3rd, 2022

KATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha majengo ya shule hapa Nchini,Mkurugenzi wa Kampuni ya Ukandarasi ya GAJOVU Joseph Ngonyani(WAYA)amechangia mifuko 20 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi 300,000 kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule ya msingi Makambi iliyopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa lengo la kuthibiti wizi na kuwaweka wanafunzi kwenye hali ya usalama.

Ngonyani alitoa msaada huo jana baada ya kusomewa taarifa fupi ya mafanikio na changamoto zinazoikabili shule hiyo na mmoja wa wahitimu wa darasa la saba Julieth Kinunda katika mahafali ya shule ya msingi Makambi ya mjini humo.

Alisema kuwa katika kuguswa na changamoto hiyo pia atatoa gari ya kampuni yake bure kwa ajili ya kubebea matilio ya ujenzi wa uzio huo pindi shughuli hiyo itakapoanza.

Akizungumza katika mahafali hayo Ngonyani amewataka wahitimu hao wa darasa la saba kutobweteka na elimu waliyoipata na badala yake wajiendeleze hadi kufikia ngazi ya chuo kikuu.

Aidha amewataka wazazi na walezi wa wahitimu hao ambao wanatarajia kufanya mitihani yao ya kumalizia elimu ya msingi Oktoba 5 hadi 6 mwaka huu kuwalea vijana wao katika maadili mema ili waweze kujiepusha na utumiaji wa madawa ya kulevya,udungaji sindano na utumiaji wa mihadarati pindi wanaposubiria matokeo yao ya mtihani.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Faustine Mbena akiongea katika mahafali hayo amempongeza mgeni rasmi huyo kwa mchango wake huo na kwamba amewataka wazazi na walezi kujenga utamaduni wa kuchangia shughuli za maendeleo ya shule badala ya kusubiria viongozi na wageni rasmi wanaoalikwa kwenye mahafali.

Awali akisoma taarifa ya shule kwa niaba ya wahitimu wenzake Julieth Kinunda alisema kuwa shule yao inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa madawati,uchakavu wa miundombinu ya nyaya za umeme,uchakavu wa choo cha walimu pamoja na ukosefu wa uzio wa shule ambao utasaidia kuthibiti wizi na uhalibifu wa miundombinu ya shule.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.