WANANCHI mkoani Ruvuma wameshauriwa kulinda misitu na kutunza vyanzo vya maji ili vyanzo hivyo viwe endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Maliasili wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe ambapo amezitaja baadhi ya changamoto wanazokutana nazo kuwa ni uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji.
Amesema uharibifu huo kwa kiasi kikubwa unatokana na uchafuzi katika vyanzo vya maji na kusababisha upungufu wa maji katika vyanzo vingi hasa wakati wa kiangazi.
Hata hivyo Challe amesema Idara yake, inaendelea kuwaelimisha wananchi kuacha shughuli za kibinadamu karibu na maeneo ya vyanzo vya maji.
“Ili kulinda vyanzo vya maji, Bonde la ziwa Nyasa limefanikiwa kuweka mipaka kwenye vyanzo vinne ambavyo ni jumla ya hekta 43,huduma ya maji na usafi wa mazingira inategemea kwa kiasi kikubwa uendelevu wa vyanzo vya maji ambavyo vinasimamiwa na mabonde”,alisisitiza.
Mkoa wa Ruvuma unategemea maji kutoka katika mabonde matatu ambayo ni bonde la Nyasa, Ruvuma na Rufiji.
Imeandikwa na Farida Baruti kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.