WAKAZI wa kijiji cha Mandepwende na kitongoji cha Zanzibar kata ya Lwinga wilaya ya Namtumbo,wameishukuru serikali kupitia wakala wa Barabara za mijini na vijijini(Tarura) wilayani humo kukamilisha ujenzi wa daraja katika mto Kotoko ambalo limechochea uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Wamesema,kukamilika kwa daraja hilo na ufunguzi wa Barabara mpya inayounganisha kijiji hicho na maeneo ya uzalishaji,hivyo kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka shambani kwenda sokoni na kufanya shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato.
Hasibuna Lutumbo makzi wa Mandepwende alisema,kabla ya kujengwa daraja la Kotoko changamoto kubwa ilikuwa namna ya kupita katika eneo hilo kwenda upande wa pili kwani wakati wa masika ujaa maji na hivyo kuwa vigumu kwenda maeneo mengine kufuata huduma muhimu za kijamii.
Aidha alisema,kukosekana kwa Barabara ya uhakika kwa muda mrefu,kumechangia kuongezeka kwa umaskini miongoni mwao licha ya jitihada kubwa wanazofanya za uzalishaji.
“tunaishukuru sana serikali yetu ya awamu ya sita kupitia Tarura kukamilisha ujenzi wa daraja,awali eneo hili halikuweza kupitika kirahisi kutokana na kujaa maji,tunawapongeza sana wataalam wetu kutoka Tarura kukamilisha kazi kwa haraka na kwa viwango”alisema.
Mwajuma Athuman alisema,awali akina mama wajawazito waliteseka pindi wanapotaka kwenda kliniki kwani walilazima kuwabeba wajawazito kwenye machela jambo lililopelekea baadhi yao kupoteza maisha kabla ya kufikishwa kwenye vituo vya kutolea huduma.
Saidi Mtawanyi,ameiomba serikali kuu kuiongezea Tarura fedha za kujenga kipande cha Barabara kilichobaki ili kurahisisha mawasiliano kati ya Kitongoji maarufu cha Zanzibar chenye idadi kubwa ya watu na kijiji cha mama cha Mandepwende.
Alisema,hatua hiyo itasaidia kuunganisha mawasiliano ya barabara kati yam kitongoji hicho na maeneo mengine ya wilaya ya Namtumbo ambayo ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilayani Namtumbo Mhandisi Fabian Lugalaba alisema,ujenzi wa daraja hilo umegharimu kiasi cha Sh.milioni 50 na ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 98 na limeanza kupitika.Alisema,daraja hilo ni sehemu ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Lwinga,Mandepwende Msengenengem na ufunguzi wa barabara mpya ya Mfwate hadi Msengenengem yenye urefu wa kilomita 41 ambayo inayohusisha na ujenzi wa box kalavati 2 ambapo gharama za mradi wote ni Sh.milioni 638.Alisema,kwa sasa ufunguzi wa barabara yote kilomita 41 umekamilika na kazi inayoendelea na ujenzi wa box kalavati mbili na mradi unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu ili kuruhusu shughuli na maisha ya wananchi kuendelea kama kawaida.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.