• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WANANCHI waishukuru serikali kwa huduma ya kifua kikuu

Imewekwa kuanzia tarehe: August 19th, 2022

BAADHI ya Wakazi wa kijiji cha Angalia kata ya Mtina wilayani Tunduru,wameishukuru wizara ya afya kupitia Hospitali ya wilaya ya Tunduru chini ya kitengo cha kifua kikuu na ukoma kwa kuwafikishia huduma ya uchunguzi  ya ugonjwa wa kifua kikuu  katika kijiji chao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa kampeni ya uchunguzi wa ugonjwa  TB kwa watoto wadogo na watu wazima walisema, hatua ya wizara kupeleka huduma hizo katika kijiji chao ni ukombozi mkubwa na  itasaidia sana wananchi kutambua hali za afya zao.

Mwanahawa Abdala(45)alisema, katika kijiji hicho hakuna  huduma yoyote ya afya,badala yake wananchi wanalazimika kwenda kijiji cha Mtina umbali wa km 7 kufuata huduma za matibabu ikiwamo ya uchunguzi wa afya zao.

Kwa mujibu wa Mwanahawa,kufikishwa kwa huduma za uchunguzi wa kifua kikuu na ukoma katika kijij chao  na vijiji mbalimbali vya pembezoni  inaonesha namna gani serikali inavyowajali na kuthamini wananchi wake kutokana na  ukweli kwamba maeneo hayo hayafikiwi kwa urahisi na wataalam wa afya.

Alisema,katika kijiji hicho kuna watu wengi wanaougua ugonjwa huo na magonjwa mengine kwa muda mrefu, lakini wanashindwa kupata tiba sahihi kutokana na kutofikiwa na wataalam wa afya mara kwa mara.

Alisema, baadhi ya watu wamepoteza maisha kwa kutopata huduma  ya uchunguzi wa afya zao na matibabu kwa wakati,hivyo kupelekwa kwa huduma ya uchunguzi wa TB itasaidia sana kuokoa maisha ya wananchi wengi hasa vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa.Habiba Said,ameiomba serikali kupeleka wataalam wa kutosha katika maeneo ya vijijini na kuboresha huduma za afya badala ya kupeleka nguvu kubwa mjini ambako ni rahisi kwa wananchi kupata na kufikiwa na huduma hizo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Angalia Ali Mbanga alisema,katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya,wameaanza ujenzi wa zahanati  ambayo ipo hatua ya kupaua baada ya serikali kutoa fedha.

Hata hivyo,amewaomba wananchi na wadau mbalimbali kujitolea katika kazi ujenzi wa zahanati hiyo kwa kuwa serikali haiwezi kutekeleza kila jambo pekee yake kutokana na majukumu iliyonayo.

Ameupongeza uongozi wa Hospitali ya wilaya Tunduru kwa uamuzi wa kupeleka wataalam kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya za wananchi hususani wenye maradhi ya kifua kikuu na ukoma.

Kwa upande wake Mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaa ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema,katika mkoa wa Ruvuma  wilaya ya Tunduru ndiyo inayoongoza kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu.

Alisema,hali hiyo inatokana na baadhi ya maeneo kuwa na makazi duni kutokana na ugumu wa maisha kwa wakazi wake na unywaji wa maziwa ya ng’ombe yasiyochemshwa vizuri.

Alisema,wanaendelea na kampeni ya kupambana na ugonjwa huo kwa watoto wadogo na watu wazima katika maeneo mbalimbali hasa vijijini na wale wanaobainika kukutwa na Tb wanaanzishiwa Dawa.

Dkt Kihongole ambaye ni mratibu wa tiba asili na mbadala wa wilaya hiyo,ameiomba jamii kutowatenga wagonjwa wa kifua kikuu,badala yake kuwapa ushirikiano na kuwapeleka katika vituo vya kutolea huduma ili waweze kupata  matibabu yanayotolewa bure katika zahanati,vituo vya afya na Hospitali zote za serikali na binafsi hapa nchini.

Dkt Kihongole alitaja dalili za ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto ni kupungua uzito,kulia lia bila sababu,makuzi duni na kwa watu wazima kukohoa  zaidi ya wiki mbili,kutokwa na jasho jingi nyakati za usiku,kukohoa damu,kukonda,kupungua uzito na kupoteza hamu ya kula.

Alisema,kinga mojawapo ya kuzuia kupata ugonjwa huo kwa watoto wadogo ni mama wajawazito  kuhakikisha wanajifungulia Hospitali ambapo baada ya mtoto kuzaliwa anapata chanjo maalum ya kuzuia maambukizi ya magonjwa mbalimbali,kuepuka kukaa kwenye mikusanyiko,kuishi kwenye nyumba yenye mwanga na hewa ya kutosha.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.