Wanchi wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,wameishauri Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuboresha Bustani ya wanyamapori Ruhila Zoo ili kushawishi na kuvutia watu wengi zaidi kwenda kutembelea bustani hiyo ya wanyama.
Wamesema,licha ya Mamlaka ya Udhibiti wa Wanyamapori Tanzania(Tawa) kanda ya Kusini kupeleka wanyama,lakini katika eneo hilo kuna changamoto nyingi ambazo serikali inatakiwa kuzifanyia kazi ili bustani ya wanyamapori Ruhila iwe chanzo kikubwa cha mapato ya Serikali.
Aidan Komba,Mkazi wa mtaa wa Mshangano katika Manispaa ya Songea alisema,bustani ya Ruhila ikiboreshwa kwa kuwekwa miundombinu mizuri na rafiki kama maeneo mengi ya kucheza watoto,mabwawa ya kuogolea na kutembea kwa mitumbwi na wanyama wa kila aina itawashawishi watu wengi kutembelea tofauti na ilivyo sasa.
Agostino Nombo,ameiomba Serikali kutupia jicho bustani ya wanyamapori Ruhila kwa kuweka mazingira mazuri ili kuwavutia watu kwenda kuona vivutio mbalimbali vilivyopo kama vile wanyama,ndege na miti aina mbalimbali iliyozunguka kwenye bustani hiyo iliyoanzishwa tangu mwaka 1973.
Helen Kavishe,ameipongeza TAWA kwa kuleta wanyama mbalimbali katika Bustani ya Ruhila Zoo ambapo alieleza kuwa, sasa wananchi wa Ruvuma hususani wanaoishi katika manispaa ya Songea wamepata sehemu nzuri ya mapumziko na kuwataka wananchi wenzake kuhakikisha wanakwenda kutembelea bustani hiyo ili waweze kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo.
Serikali kupitia mamlaka ya usimamizi Wanyamapori Tanzania(TAWA) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeleta Simba wawili majike waliopewa majina ya Lucy na Liana katika Bustani hiyo kutoka Hifadhi ya Wanyamapori ya Seva jijini Arusha ili kuchochea utalii wa ndani.
Bustani hiyo imeanzishwa kwa ajili ya wananchi wa mkoa wa Ruvuma na Watanzania kwa ujumla, kama mkakati wa Serikali ya mkoa wa Ruvuma katika kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Lengo la kuanzishwa kwa Bustani ya Wanyamapori Ruhila iliyopo katika Manispaa ya Songena yenye wanyama aina mbalimbali kama vile Pofu,nyumbu Pundamilia,kakakuona,sungura,nyani,kuro na swalapala ili wananchi waweze kupata sehemu maalum ya kupumzika ambapo mbali na.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.