Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh, Filberto Sanga tarehe 17/05/2023 akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama na wataalam wa Wilaya ya Nyasa, amefanya kikao na kikosi Cha kutunza na kutumia raslimali za uvuvi ( BMU) wavuvi,wachuuzi na viongozi wa Kata na vijiji mwambao mwa ziwa Nyasa.
Lengo la kikao hicho ni kukubaliana jinsi Ziwa Nyasa Linavyoweza kuongeza mapato,na kuacha uvuvi haramu.
Akifungua Kikao MH.Sanga amesema amelazimika kuitisha kikao hicho ili kutoa elimu na kufanya makubaliano na wavuvi na watumiaji wa raslimali za uvuvi ili kuongeza tija kipato Cha mtu mmoja na Taifa Kwa ujumla.
Ameongeza kuwa ili Wilaya iweze kuendelelea ni lazima tuwe na vikao vya kupeana uzoefu Na kuwataja wampe uzoefu jinsi Hali ilivyo na Serikali iwasaidie nini.
Wavuvi wamemshukuru MKuu wa Wilaya ya Nyasa Kwa kufanya kikao na wamemwomba kuboresha zana za uvuvi ili ziwe za kisasa ombi ambalo limepokelewa na mkuu wa Wilaya ya Nyasa na kuwataka wajisajili katika vyama vya ushirika vya wavuvi,ili waweze kupata mikopo mbalimbali ya Serikali.
Hata hivyo kikao hicho kimekubaliana , wavuvi wote wenye Nyavu haramu kuZisalimisha ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya Leo,mara baada ya hapo msako mkali utaanza na kuwafikisha mahakamani wale wote watakaokamatwa na Nyavu haramu.
Aidha Kila mvuvi awe mlinzi wa mwenzie na atoe taarifa pale anapoona Kuna mvuvi anatumia Nyavu haramu.
Viongozi wa Kata na vijiji waendelee kutoa Elimu Kwa wananchi na wavuvi ili kuzuia uvuvi haramu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.