• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WATENDAJI Ruvuma waaswa kushirikisha jamii kwenye miradi ya maendeleo

Imewekwa kuanzia tarehe: July 26th, 2023

WITO umetolewa kwa viongozi wa  na watumishi wa umma nchini,kuacha tabia ya kukumbatia madaraka wanapoanza michakato ya kuibua na kutekeleza miradi ya maendeleo yenye lengo la kuboresha huduma  za kijamii na kupunguza kiwango cha umaskini hapa nchini.

Badala yake wameombwa kuishirikisha  jamii  kwa kila hatua,ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kuharakisha kukua kwa uchumi hasa katika maeneo ya pembezoni.

Hayo yamesemwa na Mshauri mwelekezi(Consultant) wa masuala ya Utawala  bora na uwajibikaji Mnung’a Shaibu wakati wa mafunzo ya kuzijengea uwezo kamati za Pets kuhusu ushiriki na uwajibikaji wa wananchi katika serikali za mitaa.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika katika chuo cha Top One mjini Songea, yamelenga kuwajengea uelewa washiriki hao kuhusu Dhana ya utawala bora,haki na wajibu na ushiriki wa wananchi katika serikali za mitaa,vitongoji na vijiji hapa nchini.

Mnung’a alisema,suala ushirikishwaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo  kati ya jamii na viongozi ni jambo muhimu kwani linasaidia  miradi kutekelezwa kwa ubora na kwa wakati sahihi na wananchi wanakuwa sehemu ya walinzi wa miradi hiyo.

Alieleza kuwa,uzoefu unaonyesha miradi mingi inayotekelezwa kwa kuishirikisha jamii imefanikiwa kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na ambayo imetekelezwa na upande mmoja wa serikali tena kwa gharama kubwa.

“kuna tabia inayoendelea viongozi wa serikali waliopewa dhamana ya kusimamia shughuli na miradi ya maendeleo katika maeneo yetu kutumia mabavu na maamuzi  binafsi kwenye utekelezaji wa miradi,hali ambayo imesababisha baadhi ya miradi kutokamilik kwa wakati”alisema.

Ametoa wito kwa jamii wakiwemo wajumbe wa mradi PETS, kuisaidia serikali katika kuibua na kushiriki kikamilifu ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao badala ya kubaki nyuma.

Aidha,amewataka wajumbe wa mradi wa PETS kuwa na tabia ya kujisomea na kujifunza mambo mbalimbali ili kuwa na uelewa wa kutosha  wanapokwenda kufuatilia ubadhilifu wa rasilimali za umma na miradi  inayotekelezwa katika maeneo yao.

Naye Mshauri wa masuala ya sheria wa Roa James Simon,amewataka  washiriki wa mafunzo hayo kwenda kuwasaidia wananchi kufahamu mapato na matumizi,fedha zinazokusanywa na miradi inayopelekwa katika vijiji vyao.Amewaomba kwenda kuwa sehemu ya  jamii na kushiriki katika hatua zote za utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo na kuepuka kuwa kikwazo kwa kukwamisha mipango  mbalimbali iliyowekwa na serikali iliyopo madarakani.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.