Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mheshimiwa Julius Mtatiro ameaagiza watendaji wa kata na vijiji kuendelea kurekebisha viashiria vya chini vya lishe ili kupunguza changamoto ya utapiamlo na udumavu.
Mtatiro ametoa maagizo hayo wakati anazungumza kwenye kikao cha kawaida cha kujadili utekelezaji wa mkataba wa afua za lishe mjini Tunduru.
“Wekeni mkazo umuhimu wa watoa huduma za afya na kutembelea kaya zenye wajawazito na watoto chini ya miaka mitano mara kwa mara ili kuwapa elimu ya lishe bora na kufuatilia afya zao’’,alisisitiza.
Amesema ushirikiano baina ya viongozi, watendaji na wadau wote wa lishe bora itawezesha wananchi kupata elimu endelevu ya lishe na kuwa na afya bora.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe Kaimu Afisa Lishe wa Wilaya wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Martin Kigosi,ameitaja kata ya Matemanga kufanya vizuri zaidi katika utekelezaji wa mkataba huo hali ambayo imesababisha kata hiyo kupewa cheti cha pongezi na zawadi ya pesa kiasi cha shilingi laki moja.
Wakizungumza katika kikao hicho, baadhi ya wajumbe wamependekeza mikakati mbalimbali ya kuboresha lishe katika wilaya ya Tunduru.
Wameitaj Mikakati hiyo kuwa ni Pamoja na, Kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayofanya kazi katika sekta ya lishe, Kuanzisha bustani za mboga mboga katika kaya na shule na Kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa lishe borapichani kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro akizungumza kwenye kikal cha utekelezaji wa afua za lishe
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.