• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WATENDAJI wa AMCOS wapata mafunzo ya uandaaji wa vitabu na mbinu za kupata hati safi

Imewekwa kuanzia tarehe: September 21st, 2021

KATIBU Tawala msaidizi Uzalishaji na Uchumi Mkoa wa Ruvuma Jeremia Sendoro amefungua mafunzo ya uandaaji wa vitabu na Mbinu za kupata hati safi kwa wahasibu na waandishi wa AMCOS kanda ya Kusini.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo hayo  amesema Mafunzo ya wahasibu na waandishi wa vyama vya Ushirika wa Mazao na Masoko (AMCOS)  yamejumuisha mikoa ya Lindindi,Mtwara, Ruvuma na Mbeya  na kufanyika katika ukumbi wa SUT SACCOS Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

“Elimu na Mafunzo ni moja kati ya Misingi saba ya Ushirika ya Kimataifa, hivyo mafunzo ni utekelezaji  wa msingi katika kuimarisha vyama vya ushirika kwa lengo la kuvifanya  vyama kuwa na hati safi “.

Sendoro amesema Ushirika utakuwa na maana kwa Taifa ikiwa utaongeza uzalishaji na kurahisisha masoko ya Uhakika ya mazao,na hatimaye kushinda vita dhidi ya umaskini.

“Naomba niwakumbusheni kuwa ushirika ni dhana muhimu ya kujenga uchumi imara na wenye nguvu katika kupunguza na kama si kuondokana kabisa  na mfumo wa ushirika ni mfumo pekee na muhimu wa kupambana  na vita dhidi ya uchumi”.

Sendoro amesema Serikali inatambua,Ushirika ni dhana pekee ya kumkomboa mkulima na mnyonge kiuchumi ,Ushirika umeelekezwa katika ilani ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi (CCM) ya  mwaka 2020 hadi 2025 kuwa ni nyenzo muhimu ya kukuza Uchumi.

Katibu Tawala msaidizi ametoa wito  kwa viongozi na watendaji wa vyama vya Ushirika kuwa karibu na wakulima wakati wote wa shughuli za msimu ili kubaini na kutatua changamoto mbalimbali za utekelezaji  wa shughuli za masoko,kusimamia na kuhakikisha wakulima wote wanauza mazao kupitia mifumo iliyoelekezwa na Serikali.

Kwa upande wake Afisa mipango Emmanuel  Danda amesema kuwa changamoto zinazosababisha  wanachama kupata hati chafu  ni elimu katika eneo la uhasibu kupelekea   kuwa na hati chafu kwa vyama vya ushirika.

Danda amesema kwa msimu huu na ujao wamejipanga kwa kutafuta wadau ili waweze kuimarisha masoko na kuwajengea uwezo watendaji ili mifumo ya vyama vya ushirika iweze kufanya vizuri kwa wakulima.

Mwenyekiti wa Mafunzo hayo Hamza Rashi Mbutuka akisoma Risala kwa mgeni rasmi amewapongeza waandaji wa mafunzo ambao ni wakufunzi kutoka chuo cha Ushirika Moshi,Chuo cha uhasibu na maafisa ushirika kutoka Wilaya mbalimbali zilizomo ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma

Septemba 21,2021.

 

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.