WATOTO 289 walio chini ya umri wa miaka 0-14 walikutwa na maambukizi ya ugonjwa wa kifau kikuu mwaka 2021 katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema hayo kwa nyakati tofauti, wakati wa kampeni za uchunguzi wa ugonjwa huo kwa watoto inayoendelea katika vijiji mbalimbali wilayani humo.
Alisema kati yao, watoto walio chini ya umri wa miaka 0-4 walikuwa 29 sawa na asilimia 56, miaka 5-9 walikuwa 32 sawa na asilimia 4.17 na kuanzia umri wa miaka 10-14 walikuwa 30 sawa na asilimia 3.19.
Mkasange alisema, kwa mwaka 2021 lengo ilikuwa kuibua wagonjwa 741,hata hivyo walivuka lengo na kufanikiwa kuibua wagonjwa 768.
Ameishukuru Serikali na wadau mbalimbali wakiwamo Shirika lisilo la kiserikali la MDH, kwa mchango wao uliowezesha wataalam wa kitengo cha kifua kikuu na ukoma kufanikisha kampeni hizo ambazo zimesaidia sana kuibua wagonjwa wengi.
Alisema,kutokana na ukubwa wa ugonjwa huo wilayani Tunduru,serikali kupitia Hospitali ya wilaya kitengo cha kifua kikuu na ukoma wameanzisha kampeni ya kupita kila kijiji na badaye kila nyumba ili kufanya uchunguzi kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Dkt Mkasange alisema, baada ya watoto wataendelea kwa watu wazima na watakaobainika kuwa na ugonjwa ho wataanzishiwa dawa papo hapo ili jamii ya watu wa Tunduru iwe salama na kushiri vyema ujenzi wa Taifa.
“kampeni ya uchunguzi wa TB kwa watoto tumezindua mwezi uliopita na tumekusudia kufika kila kijiji kwa ajili ya kufanya uchunguzi kwa watoto,tunaomba sana wazazi na walezi kuleta watoto ili kufahamu afya zao”alisema Mkasange.
Alisema,kampeni hiyo ni endelevu na ya lazima kwa watoto wote walio chini ya umri huo na kuendelea kufanyiwa uchunguzi wa afya zao.
Aidha alisema, kuanzia Mwezi Januari hadi March 2022 jumla ya watu 120 kati yao 57 ni watoto wamepatikana kuwa na virusi vya ugonjwa huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.