• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WATU 35 wauawa na wanyamapori Kanda ya Ruvuma,RC azindua mradi wa kutatua migongano baina ya binadamu na wanyamapori

Imewekwa kuanzia tarehe: August 11th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amezindua Mradi wa Kutatua migongano baina ya binadamu na wanyamapori katika ukanda wa Ruvuma.

Uzinduzi wa mradi huo unaotekelezwa na  serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la (GIZ) la nchini Ujerumani umefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea  ukishirikisha wawakilishi kutoka mikoa ya Ruvuma na Lindi.

Akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo,Mkuu wa  Mkoa wa Ruvuma amesema migongano baina ya binadamu na wanyamapori ni miongoni mwa changamoto kubwa katika mikoa ya kusini  hivyo kuhatarisha Maisha ya wananchi na mali zao.

“Takwimu za mwaka mmoja pekee 2022/2023 zinaonesha kuwa wanyamapori wamesababisha vifo 35,majeruhi 17 na kuharibu takriban jumla ya hekari 10,724.05 za mazao mbalimbali ‘’’.alisema Kanali Thomas.

Hata hivyo amesema  serikali ina matarajio kuwa mradi huo ambao utatekelezwa kwa kuhusisha Jeshi la Uhifadhi wa Misitu na wanyamapori kutoka TANAPA,TFS na TAWA Pamoja na mikoa na wilaya utapunguza au kumaliza changamoto ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori.

Ameagiza mara baada ya uzinduzi huo yafanyike maandalizi ya mpango mkakati utakaoanisha mbinu za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu ambapo pia amelipongeza Shirika la GIZ  kwa kukubali kuleta mradi huo katika ukanda wa Ruvuma na kwamba mradi umekuja wakati muafaka kutokana na ongezeko la matukio la wanyamapori wakali na waharibifu.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Nchini Antonia Rafael akizungumza  kwenye uzinduzi huo,amesema Mradi huo unatekelezwa katika wilaya za Namtumbo na Tunduru mkoani Ruvuma na wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Amesema kutokana na kuongezeka kwa migongano baina ya binadamu na wanyamapori serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Amebainisha kuwa  Wizara ya Maliasili na Utalii imeingia mkataba wa kushirikiana na  Shirika la GIZ la nchini Ujerumani ili kutatua changamoto ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori katika wilaya tatu za Tunduru,Namtumbo na Liwale kwenye mikoa ya Ruvuma na Lindi.

Amesema mradi huo unatekelezwa  katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha  2022/2023 hadi 2025 na kwamba mradi unagharimu  zaidi ya bilioni 15.

Naye Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi wa TAWA Kanda ya Kusini  Keneth Sanga amezitaja wilaya zinazoongoza kwa matukio mengi ya kuvamiwa na wanyamapori ambapo katika kipindi cha mwaka huu wilaya ya Lindi inayoongoza kwa kuwa  na matukio 161,ikifuatiwa na  wilaya za Nachingwea,Liwale,Rufiji na Tunduru.

Amewataja wanyamapori wanaohusika kwenye matukio hayo kuwa ni  tembo anayeongoza kwa kusababisha matukio mengi ambapo kwa mwaka huu pekee tembo amesababisha matukio 682  akifuatiwa na simba, Nyati,kiboko,fisi na mamba.

Miongoni mwa maazimio yaliyopitishwa kwenye uzinduzi huo ni Pamoja  na kuandaa mapema mpango shirikishi wa utekelezaji wa mpango huu  ili kutatua changamoto hiyo katika ukanda wa Ruvuma.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.