AIDI ya wazazi 763 wamekamatwa katika operesheni maalum ya nyumba hadi nyumba, ya kuwasaka wazazi na walezi wasiopeleka watoto wao waliochaguliwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu katika wilaya yaTunduru mkoani Ruvuma.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro amesema,kukamatwa kwa wazazi hao kumetokana na muda wa siku 14 waliopewa kupeleka watoto shule kwa hiari kumalizika licha ya uhamasishaji mkubwa uliofanywa na viongozi wa serikali,kamati ya ulinzi na usalama na madiwani.
Kwa mujibu wa Mtatiro,msako huo unafanyika usiku na mchana,na ni mkakati wa kuwapata watoto wote 5,869 waliomaliza darasa la saba mwaka jana na kuchaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza,lakini hadi mwishoni mwa wiki iliyopita wamebaki nyumbani.
Aidha amesema,katika msako huo wazazi wengine 600 wamejisalimisha kwa kupeleka watoto wao shule baada ya kushuhudia wenzao wamekatwa na kufikishwa polisi kwenye operesheni inayoendelea katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Mtatiro alisema,operesheni hiyo imekuwa yenye mafanikio makubwa kwani katika muda wa siku tatu wamewapeleka zaidi ya watoto 1,335 shule kati ya 5,868 wanaotakiwa kuanza kidato cha kwanza na wanaendelea kuwatafuta watoto waliobaki.
Mtatiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Tunduru alisema,watahakikisha hadi Jumatatu ya wiki ijayo watoto wote wanaotakiwa kuanza kidato cha kwanza katika muhula wa masomo ulioanza tangu tarehe 9 Januari wanaripoti kwenye shule walizopangiwa.
“tunendelea kuwasaka na kuwachukulia hatua za kisheria wazazi na walezi ambao baada siku 14 tulizowapa za maandalizi ya watoto wao kupita lakini wameshindwa kutumia fursa hiyo vizuri,tunataka vijana wote wanaotakiwa kuanza kidato cha kwanza katika wilaya yetu wanaripoti kwenye shule walizopangiwa na sio vinginevyo”alisema Mtatiro.
Alisema,serikali ya awamu ya sita imetoa fedha nyingi za kujenga shule mpya, kuongeza madarasa mapya kwa baadhi ya shule za zamani,kununua meza na viti na kusimamia sera ya elimu bila malipo kuanzia darasa la awali hadi kidato cha sita.
Alisema,licha ya serikali kukamilisha ujenzi wa shule mpya na vyumba vya madarasa kwa asilimia 100,lakini inasikitisha kuona mpaka baadhi ya wanafunzi bado wako nyumbani huku wazazi wao wakitoa visingizio visivyokuwa na msingi.
Amewakumbusha wazazi na walezi wilayani humo kutambua kuwa,muda wa kupeleka watoto shule kwa hiari umepita na sasa wanatakiwa kupeleka kwa lazima na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani.
“hakuna kikwazo kwa wazazi kushindwa kupeleka watoto shuleni,serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa kwa kutengeneza madawati,viti na meza ambazo awali mzazi alilazimika kutumia kati ya Sh.80,000 hadi 100,000, lakini vifaa hivyo vinapatikana bure shuleni”alisema.
Mkuu huyo wa wilaya,amewaasa watoto waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu, kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kusoma kwa bidii kama njia itakayo wawezesha kutimiza ndoto zao pindi watakapokuwa watu wazima na kamwe wasikubali kufanyishwa kazi za nyumbani kama kuchunga mifugo na kazi za ndani.
Alisema,tunapohitaji maendeleo katika nchi yetu suala la uwekezaji wa elimu ni jambo muhimu sana, ndiyo maana serikali imeamua kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne ni ya lazima,kwa hiyo wazazi na viongozi wana wajibu kuhakikisha watoto wote wanakwenda shule na wanafikia malengo yao.
Baadhi ya wazazi waliokamatwa katika opresheni hiyo,wameoimba serikali iwaongezee muda wa kupeleka watoto shule ili waweze kufanya maandalizi ya watoto kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.
Rehema Waziri alisema,licha ya serikali kuagiza watoto waende shule hata kama hawana mahitaji yote muhimu,lakini kama mzazi bado ana wajibu kumpatia mtoto wao mahitaji ya shule ikiwamo sare na madaftari badala ya kuitegemea serikali kufanya kila kitu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.