WAZIRI wa Maji Mhe, Jumaa Hamidu Aweso amewataka viongozi wa bodi ya maji Mkoani Ruvuma kuwashirikisha wananchi kulinda vyanzo vya maji
Waziri Aweso alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma, kwenye Hafla ya uzinduzi wa bodi ya sita ya bonde la Ziwa Nyasa katika ukumbi wa Heritage cottage mjini Songea
Alisema ni vizuri wananchi washirikishwe kwa kuwapa elimu ya ulindaji wa vyanzo ili kuweza kuondokana athari za ukosefu wa maji pia amewataka wakurugenzi wa mamlaka ya maji kutambua majukumu yao ya msingi asa kutambua vyanzo pamoja na kuvipa kipaumbele kwa kuwashirikisha wananchi.
“Vyanzo vyote vya maji vinapita kwenye Jamii na kila eneo kuna Wananchi kama kiongozi wenu nimejifunza kuwa Jamii ipo tu siku zote ukiishirikisha mtafanikiwa na msipo ishirikisha mtakwama kama kiongozi wenu naomba tushirikiane na jamii tutafanikiwa kulinda vyanzo vya maji” alisema Aweso.
Hata hivyo amewasisitiza viongozi wa bodi hiyo ya sita bonde la Ziwa Nyasa ikasimamie rasilimali za Maji kwani serikali inawekeza fedha nyingi kwenye miradi hiyo ya Maji kwa lengo la kupunguza chamgamoto za maji na kulinda vyanzo vya vyake.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemshukuru Mhe, Rais Samia Suluhu kwa kutoa fedha za miradi ya Maji yenye thamani ya shilingi bilioni 42 ambayo inatekeleza ujenzi wa miradi 35 mkoani umo
“Tunamshukuru sana Mhe, Rais kwa kutambua shida zetu na kweli kwa dhati ya moyo wake ameamu kuwatua akinamama wa Mkoa wa Ruvuma ndoo kichwani pia sisi kama serikali ya Mkoa tutazidi kusimamia na kulinda vyanzo vyanzo vya Maji” alisema kanali Thomas
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Odo Mwisho alisema wao kama chama watazidi kushirikiana na bodi pamoja na mamlaka ya maji RUWASA ili kuwaamasisha Wananchi katika kuitunza na kuilinda vyanzo vya Maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.