Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mheshimiwa Jenista Mhagama amewataka wazazi kutenga muda wa malezi kwa watoto ili wawe na maadili mema.
Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 69 ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi yaliyofanyika katika Kijiji cha Kilagano Jimbo la Peramiho.
Waziri Mhagama amesema, mtoto anayelelewa kwa kuangalia mfano mzuri wa baba na mama atakuwa na nidhamu na tabia njema.
“Wazazi tutafakari utaratibu tunaotumia kulea watoto wetu ili wawe na madili bora katika katika Jamii,kizazi kipya kimeathirika na masuala ya utandawazi,nguvu mpya ya Mawasiliano isipotumika vizuri itakuwa ni chanzo cha upotofu wa maadili,” alisema Waziri Mhagama.
Amelitaja lengo la kuanzishwa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha inajenga maadili mema ndani ya chama na taifa kwa ujumla.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.