Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amempongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Damian Dallu kwa kuadhimisha jubilei ya miaka 125.
Amesema katika kipindi chote hicho kanisa limefanikiwa kuwajenga waumini wake kiimani na kuwaelimisha namna waumini wanavyoweza kukuza uchumi wa mtu binafsi.
Waziri Mkuu alikuwa anazungumza kwenye kilele cha Jubilei ya miaka 125 ya uinjlishaji wa kanisa katoliki Jimbo Kuu la Songea iliyofanyika Abasia ya Peramiho nje kidogo ya mji wa Songea ambapo Waziri Mkuu alikuwa ni mgeni rasmi
Ameongeza kuwa katika kipindi hicho kanisa limekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kwa vitendo jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo kwa kujenga shule,vituo vya afya,viwanda,vituo vya kulelea Watoto yatima,kuanzisha vyuo mbalimbali vya ufundi stadi na kuanzisha vyuo vikuu ambapo amesisitiza kuwa kazi hiyo imeleta maendeleo makubwa katika ustawi wa jamii.
Awali akizungumza kabla ya Waziri Mkuu kuzungumza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Damian Dallu amesema kanisa linaadhimisha jubilei ya uinjilishaji iliyoletwa na wamisionari wabenediktini mwaka 1898 likiwa limepata mafanikio makubwa kimwili na kiroho kutokana na wamisionari wabenediktini kupanda mbegu ya injili iliyozaa matunda kwa kipindi cha miaka 125.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.