WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Oktoba Mosi kwenye Jubilei ya miaka 125 ya uinjlishaji jimbo kuu la Songea.Maadhimisho hayo yanafanyika Abasi ya Peramiho nje kidogo ya mji wa Songea.
Waumini wote wa Jimbo Kuu la Songea pamoja na Waamini kutoka katika Kila Jimbo ndani na nje ya Tanzania mnakaribishwa kwenye sherehe ya Jubilei ya miaka 125 ya Unjilishaji jimboni Songea. Misa ya Sherehe hiyo ya Jubilei itaanza saa 4;00 asubuhi kamili siku ya Jumapili Abasi ya Peramiho.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas Septemba 30 aliwaongoza wakazi wa Wilaya ya Songea na Mkoa wa Ruvuma kumpokea Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Ndege wa Songea wakati anawasili kwa ajili ya kushiriki kwenye Jubilei hiyo ambayo inahudhuriwa na wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.