• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAZIRI Ndalichako aziagiza Halmashauri nchini kutenga bajeti ya mafuta kinga kwa wenye ualbino

Imewekwa kuanzia tarehe: June 13th, 2023

Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na  Watu wenye Ulemavu Prof.Joyce Ndalichako  ameziagiza Halmashauri zote nchini kutenga bajeti ya mafuta kinga kwa ajili ya watu wenye ualbino.

Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo wakati anazungumza kwenye hotuba yake iliyosomwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelewa kuhusu ualbino yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

“Ninafahamu mafuta kinga yameingizwa katika mnyororo wa ugavi wa manunuzi ya dawa wa MSD,ninatambua kuwa upatikanaji wa mafuta haya unaweza kuwa si toshelevu,tengeni bajeti na  ofisi yangu itafanya ufuatiliaji wa karibu wakati wote kwenye vituo vya afya’’,alisisitiza Ndalichako.

Amesema Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 ilitenga bajeti ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa mafuta kinga kwa watu wenye ualbino nchini.

Hata hivyo amesema katika eneo la afya serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga vituo vya kutolea huduma za afya vilivyo na miundombinu rafiki  kwa watu wenye ulemavu.

Amesisitiza kuwa serikali imeendelea kuyapa kipaumbele masuala ya watu wenye ulemavu ikiwa ni Pamoja na masuala ya elimu,uwezeshaji wa kiuchumi,afya,ajira,nyenzo za kujimudu na mafunzo ya ufundi stadi.

Amebainisha zaidi kuwa serikali inatambua kuwa watu wenye ualbino bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali na kwamba serikali imedhamiria  kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu nchini wanapata haki zao za msingi Pamoja na ustawi wa Maisha yao ya kila siku ndani ya familia na jamii inayowazunguka.

Amesema serikali imeendelea kufufua vyuo vya ufundi stadi na kufanya marekebisho kwa ajili ya mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 serikali inaendelea kutekeleza miradi ya ujenzi wa vyuo vipya na marekebisho ya vyuo vya ufundi stadi katika mikoa ya Ruvuma,Songwe na Kigoma.

Ameongeza kuwa serikali imeendelea kuajiri vijana wenye ulemavu katika kada mbalimbali ambapo kuanzia mwaka 2020 hadi 2023 serikalini imeajiri watumishi wenye ulemavu  812 na kwamba katika programu ya ukuzaji ujuzi kuanzia mwaka 2021 hadi 2023 jumla ya vijana wenye ulemavu 569 wamepatiwa mafunzo.

Waziri Ndalichako pia amewaagiza maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha takwimu za watu wenye ualbino zinapatikana katika maeneo yao kwa ajili ya kupata huduma muhimu.

Awali risala ya watu wenye ualbino kwenye maadhimisho hayo iliyosomwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wwenye ulemavu nchini Erenest Kimaila imezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni upatikanaji wa vifaa kinga vya kudhibiti saratani ya Ngozi kwa wenye ualbino ikiwemo mafuta kinga na vifaa vya upasuaji baridi (cryosurgery equipment).

Haya ni maadhimisho ya 17 kitaifa na maadhimisho ya saba kitaifa kwa watu wenye ualbino yenye kauli mbiu ujumuishi ni uimara(inclusion is strength).

 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wwenye ulemavu nchini Erenest Kimaila akizungumza kwenye maadhimisho ya siku  kimataifa ya siku ya uelewa kuhusu watu wenye ualbino

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.