• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAZIRI Ndalichako akagua mradi wa bilioni moja kwa ajili ya wenye ulemavu Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: August 25th, 2023

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amekagua mradi wa  watu wenye ulemavu katika Kijiji cha Liganga wilayani Songea mkoani Ruvuma unaotarajia kugharimu shilingi bilioni moja hadi kukamilika.

Profesa Ndalichako amekagua mradi huo wa Chuo cha Ufundi Stadi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu unaotekelezwa kwa njia ya force account ambao unatarajia kukamilika Oktoba 30 mwaka huu.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo kwa Waziri Ndalichako,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Neema Maghembe amesema mradi huo unatekelezwa katika awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza inajengwa miundombinu ya vyumba kumi vya madarasa na bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40.

Maghembe ameongeza kuwa katika awamu hiyo pia inajengwa nyumba moja yenye uwezo wa kuchukua familia tatu ambapo amesema wanatarajia kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Amezitaja changamoto zilizopo kwenye mradi huo kuwa ni ukosefu wa maji ya kutosha kutokana na chanzo cha maji kuwa mbali na eneo la mradi,kuongezeka kwa gharama za vifaa na gharama ya usafirishaji kutoka mjini Songea.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo Waziri Prof.Ndalichako  amepongeza usimamizi mzuri wa mradi huo hali ambayo amesema imesababisha kuwa na ubora wa majengo yanayoendana na thamani ya fedha.

“Nimekagua majengo ya mradi huu nimegundua mradi unatekelezwa  katika viwango na ubora wa juu,naamini mradi utakamilika ndani ya muda uliopangwa’’,alisisitiza Prof.Ndalichako.

Waziri Ndalichako ameahidi kushughulikia changamoto zote zilizojitokeza ili kuhakikisha mradi huo unakamilika na kuanza kuwahudumia watu wenye ulemavu.

Amelitaja lengo la Rais Dkt.Samia kutoa fedha za kujenga chuo hicho ni kutoa fursa ya ufundi stadi kwa watu wenye ulemavu na kufanya marekebisho ili kuwapunguzia makali ya ulemavu ili waweze kuchangia maendeleo ya Taifa.

Waziri Profesa Ndalichako amefanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Ruvuma kwa kutembelea wilaya ya Songea.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.