Machifu nchini wamepongezwa kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuungana na Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kuimarisha amani na Utulivu nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas Mkoani Ruvuma alipokutana na Machifu kutoka makabila mbalimbali ya hapa nchini waliofanya ziara ya kutembelea Makumbusho ya Taifa ya Majimaj Mjini Songea yaliyosheheni historia ya harakati za kupigania uhuru wakiwemo mashujaa wa vita ya Majimaji 67 walioua kikatili na wajerumani kwa kunyongwa mwaka 1906.
Ziara hiyo ya machifu ni sehemu ya Maandalizi ya mapokezi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuitembelea Makumbusho hiyo Septemba 23 mwaka huu.
Mhe. Chana aliwahakikishia Machifu hao kuwa Wizara anayoingoza itaendelea kushirikiana nao kikamilifu katika Uhifadhi na kuendeleza urithi wa Kihistoria nchini ili watanzania waweze kunufaika na Mazao hayo ya Utalii wa Historia na Malikale.
Pamoja na kukutana na Machifu hao, Mhe. Balozi Chana amekagua maandalizi ya mapokezi ya Mhe. Rais Samia kwenye Makumbusho hiyo iliyohifadhi Historia adhimu na adimu katika ukombozi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla dhidi ya Ukoloni Miaka takribani 119 iliyopita.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.