WILAYA ya Nyasa mkoani Ruvuma bado ina fursa za maliasili ya kutosha zikiwemo misitu, wanyamapori, samaki, mito, ziwa, fukwe na mali kale ambazo hazijaharibiwa ndiyo maana tunasema wilaya ya Nyasa ni benki ya vivutio vya utalii na uwekezaji.
Fursa hizo zinaweza kutoa mchango mkubwa kwenye pato la Taifa na wananchi wa wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla kupitia utalii wa kiutamaduni na ikolojia. Makao makuu ya Wilaya ya Nyasa yapo katika Mji wa Mbambabay.
Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema wilaya hiyo ina sifa ya kuwepo kwenye bonde la ufa, ambapo bonde hilo huanza kuonekana kutoka katika maeneo ya Buruma, unaposhuka milima katika kona zinazoitwa Ambrosi.
Moja ya kivutio adimu cha utalii katika wilaya ya Nyasa ni uwepo wa Ziwa Nyasa ambalo linapatikana Kusini – Magharibi mwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani,ni la tatu kwa ukubwa barani Afrika.
Ziwa hilo lina kina cha kati ya mita 426 na 758 na hii ni kutokana na kupitiwa na bonde la ufa. Kwa upande wa Tanzania mito mingi inapatikana ikitokea wilaya ya Nyasa katika safu za milima ya Livingstone, mito hiyo ni Ruhuhu, Lumeme, Ruhekei, Lwika, Mbamba Bay, Likumbo na Chiwindi ambayo huingiza maji ndani ya Ziwa Nyasa.
Ziwa Nyasa ni kuvutio kikubwa cha Utalii kanda ya kusini kwa kuwa limesheheni vitu vingi ndani yake na tabia tofauti ukilinganisha na maziwa mengine ya hapa nchini na duniani kote.
Baadhi ya tabia za ziwa hili ni uwepo wa maji meupe na maangavu eneo lote la ziwa na mawe marefu ambayo yanajulikana kwa majina ya hia na mala yanayobeba sifa tofauti.
Tabia nyingine za Ziwa hilo ni mawimbi makubwa, fukwe nzuri na zenye sifa tofauti, mawe kuonekana kama sakafu eneo la Chiwindi, fukwe zenye udongo wa mfinyanzi, kina cha maji kuwa kifupi kwa umbali
Ziwa Nyasa ni kuvutio kikubwa cha Utalii kanda ya kusini kwa kuwa limesheheni vitu vingi ndani yake na tabia tofauti ukilinganisha na maziwa mengine ya hapa nchini na duniani kote.
Baadhi ya tabia za ziwa hili ni uwepo wa maji meupe na maangavu eneo lote la ziwa na mawe marefu ambayo yanajulikana kwa majina ya hia na mala yanayobeba sifa tofauti.
Tabia nyingine za Ziwa hilo ni mawimbi makubwa, fukwe nzuri na zenye sifa tofauti, mawe kuonekana kama sakafu eneo la Chiwindi, fukwe zenye udongo wa mfinyanzi, kina cha maji kuwa kifupi kwa umbali.
Kivutio kingine ni msitu wa Mbamba ambapo wenyeji wa Wilaya ya Nyasa, hutumia msitu wa Mbamba kwa matambiko ya kupiga ngoma za kufukuza au kuita majini kwa imani zao na kwamba katika msitu huo kuna wanyama kama chui wakitokea milima ya Nangombo, Ukuli na Chinyemba ambao wanapatikana katika rasi hiyo, wakiwafuata wanyama aina ya ngedere waliopo kwa wingi katika msitu huo.
Maeneo mengine ya vivutio vya utalii kwa Wilaya hiyo anayataja kuwa ni visiwa vya Mbamba, Lundo,Hongi na jiwe la Pomonda ambavyo vyote vimekuwa na sifa na historia nyingi ambazo zikitangazwa vizuri zitachangia kukuza utalii kwa kuvutia watalii wa ndani na nje.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.