MKUU wa wilaya ya Songea Pololet Mgema ametoa siku 30 kwa watendaji wa Halmashauri za Madaba,Songea Manispaa na Halmashauri ya wilaya ya Songea kutatua changamoto za madawati katika Halmashauri zao.
Hayo yamebainika kwenye kikao kazi cha ufuatiliaji wa miradi mbalimbali kilichofanyika 25/02/2020 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mgema, alitoa agizo hilo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri ya Madaba, Songea DC, Manispaa ya Songea ambapo alisema hadi kufikia tarehe 25/02/2020 kwa kila Halmshauri iwe imekamilisha zoezi la utengenezaji wa Madawati shule ya Msingi na Shule za Sekondari.
“kutokana na mahitaji kuwa makubwa kuliko uwezo wa Halmashauri, hivyo nawaaagiza TFS Kutoa vibali kwa ajili ya uvunaji wa miti ambayo itaisaidia katika utengenezaji wa Madawati hayo lakini mara mtakapohitaji kukata miti hiyo ni lazima taarifa ipelekwe ofisini kwa ufuatiliaji wa zoezi hilo.” Alisisitiza.
Alibainisha mahitaji na mapungufu yaliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa shule za Msingi mahitaji ya Madawati 11,584, Yaliyopo ni 10,277, Upungufu ni madawati 1,307 sawa na asilimia11. Kwa upande wa Shule ya Sekondari mahitaji ya viti ni 6,482, yaliyopo ni 4033, na pungufu ni 2449, pia mahitaji ya meza 6482, yaliyopo ni 4625 na pungufu ni 1857.
Halmashauri ya Madaba Mahitaji ya Madawati ni 531,Yaliyopo ni 578, na kufanya ziada ya madawati 62. Pia kwa upande wa Sekondari mahitaji ya meza ni 2910, yaliyopo 2891, pungufu 19 pia mahitaji ya viti ni 2910, yaliyopo ni 2831 na pungufu ya viti ni 79.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea Kwa Shule za msingi mahitaji ya Madawati 17,827, yaliyopo ni 15,580, na pungufu ni 2,247. Pia Mahitaji Ya Meza shule za Sekondari ni 15444, yaliyopo ni 9733, pungufu 5711 na mahitaji ya viti ni 15444, yaliyopo 9990, pungufu 5454.
Aidha, katika kukabiliana na changamoto hizo kiongozi huyo amezitaja njia mbadala za utatuzi wa changamoto hizo ni pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali, TFS kutoa vibali kwa ajili ya ukataji wa miti, kuwashirikisha viongozi ngazi ya kata/vijiji/ Mtaa pamoja na kuanzisha mfuko wa Elimu kwa halmashauri.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.